MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright, jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Marekani.

Akizungumza muda mfupi baada ya balozi huyo kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Aprili 11 2022, Kanali Mstaafu Kinana alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya kawaida katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo.

“Mazungumzo yetu yalikuwa yakawaida, tumezungumzia namna ya kuimarisha uhusiano pamoja na ustawi wa wananchi,” alisema Kanali Kinana.

Alisema miongoni mwa maeneo waliyoyagusia katika mazungumzo yao ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii ikiwamo afya na utoaji haki kupitia mifumo mbalimbali.

Viongozi hao wamekutana zikiwa siku chache tangu balozi huyo alipokutana na Rais Samia Suluhu Hassan.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimuaga Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright) leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright (kushoto) leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright leo katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright (kushoto) leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald J. Wright (kushoto) leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. (Picha na Fahad Siraji)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...