Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baada ya mbio za Mwenge kupitia na kujiridhisha na taratibu zote zinazochukuliwa na halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha wananchi wananufaika na mikopo,kiongozi wa mbio mbio za Mwenge kitaifa Ndugu. Sahili Geraruma amekabidhi hundi kwa vikundi 18 vya wanawake,12 vijana na 3 kwa watu wenye ulemavu yenye thamani ya Milioni 260,000,000
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi hiyo katika kijiji cha Nyombo Geraruma ametoa wito kwa kundi la vijana kuendelea kujitokeza na kuomba katika halmashauri zao kuomba na kuomba mikopo ili kujikwamua kiuchumi na kuepuka makundi yasiyofaa mitaani.
“Baada yam bio za Mwenge kuwa zimepitia,na kujiridhisha na taratibu zote zinazochukuliwa na halmashauri kuhakikisha vijana wananufaika na asilimia kumi ya mapato ya ndani,mbio hizi za Mwenge wa uhuru leo zinakabidhi hundi kwa vikundi 18 vya wanawake,vina 12 na watatu watu wenye ulemavu ni jumla ya shilingi milioni mia mbili na sitini tu”alisema Geraruma
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi.Sharifa Nabarang’anya ameishukuru serikali kwa kubadilisha sheria ya urejeshaji ya mikopo hiyo isiyokuwa na riba huku akiahidi kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya wananchi wa wilaya hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru akikagua vikundi vya wajasiriamali waliofanikiwa kupata mikopo kupitia halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akikabidhi hundi kwa vikundi wilayani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...