Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa kwa mwaka 2022 Sahili Geraruma ameongoza
zoezi la uteketezaji nyavu haramu zilizokamatwa kwa wavuvi wilayani
Ludewa mkoani Njombe zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
6,000,000.
Akichoma nyavu hizo Geraruma amewataka maafisa uvuvi
wote kutumia vyema taaluma zao kwa kuzuia uingizwaji wa nyavu hizo
ambazo zinaleta uharibifu kwa samaki waliopo ziwani.
"Nyavu hizi
zina matundu madogo sana hivyo hazifai kutumia kuvulia samaki, kwakuwa
nyavu hizi huvua samaki ambao bado wanatakiwa kuendelea kukua ni vyema
tukafuata sheria za uvuvi ili na kuvua samaki ambao tayari wamefikia
umri wa kuvuliwa".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...