.jpg)
Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB, ilieleza kwamba mchezo huo utapigwa siku ya MAJIya Aprili tatu mwaka huu katika uwanja huo wa Uhuru badala ya Azam Complex Chamanzi kama ratiba ya awali ilivyoelekeza kutokana na kukamilika kwa matengenezo yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja huo.
Kutokana na barua hiyo ya TPLB, Timu ya Manispaa ya Kinondoni inarejea sasa katika uwanja wake wa nyumbani ikiwa ni baada ya kupita kwa takribani michezo mitano ikicheza nje ya uwanja huo na hivyo kulazimika kutumia uwanja wa Azam Complex Chamanzi ambapo mara ya mwisho kutumia uwanja huo wa Uhuru ilikuwa ni kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC na KMC kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja.
KMC FC chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana hadi sasa imejiandaa vema kweye mchezo huo licha ya kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba Timu ya Namungo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake lakini ubora wa wachezaji pamoja na Benchi zima la ufundi litahakikisha kuwa alama tatu muhimu zinapatikana.
“Tumetoka kupoteza michezo miwili mfululizo, na tunakwenda kwenye mchezo mwingine tukiwa nyumbani, hii ninafasi kwetu ya kusahihisha makosa ya awali na kwamba Kocha Mkuu Hitimana katika kipindi hiki ambacho Timu zilikuwa kwenye mapumziko kupisha kalenda ya FIFA amefanya maboresho kwenye maeneo ambayo aliona yanachangamoto ambazo zilikosesha Timu kupata matokeo mazuri, hivyo mashabiki zetu watarajie kupata burudani.
Kwakipindi kirefu hatujatumia uwanja wetu halisi wa nyumbani, na sasa tunarejea kwenye mchezo dhidi ya Namungo, hivyo Tunaipongeza TPLB kwa ushirikiano mkubwa waliotuonesha kwa kipindi chote hicho na sasa tunakwenda kesho tukifahamu kabisa mchezo utakuwa mgumu lakini KMC FC tumejipanga kuondoka na alama tatu muhimu.
Aidha Klabu ya KMC FC inawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwenye mchezo huo muhimu ambao wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba wanatoa burudani iliyoambatana na ushindi, ukizingatia kuwa itakuwa siku ya wekeand.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...