Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KUFUATIA Tambo alilolitoa Msanii wa kundi la 'Konde gang', Rajabu Kahali 'Harmonize' kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Instagram) na kujigamba kuwa yuko tayari kwa pambano lolote na kuhitaji mpinzani wa kupigana nae ulingoni,wadau wa Masumbwi wameteta jambo.

Akizungunza Michuzi Tv Muandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa nchini, Meja Selemani Semunyu amesema kitendo hiko cha msanii huyo kuthamini mchezo huo kimeleta faraja sana na kuhamasisha na kuvutiwa kumkaribisha mezani kwa ajili ya kumuandalia pambano.

" Nimesikia faraja kuona msanii mkubwa "Tembo" Harmonize anasapoti mchezo wa ndondi, lakini anatamani kuzichapa siku moja na mpinzani wake yoyote anaejiamini, niko tayari kumuandalia pambano msanii huyo na ningependa kuelekea pambano la kusaka Mabondia watakaocheza pambano la utangulizi kwa mkoa wa Mtwara, " amesema Semunyu.

Pia semunyu amefafanua zaidi angependa kuona Harmonize anacheza pambano hilo katika viwanja vya CCM Nang'wanda Sijaona ambapo ni nyumbani kwao kabisa pia italeta hamasa kwa mabondia wa wanyumbani kufanya vizuri.

"Maandalizi ya pambano la kutafuta mabondia ambao watacheza mapambano ya utangulizi sikukuu ya Idd Mosi yanaendelea vizuri, " amesema Semunyu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...