Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema katika kutekeleza Diplomasia ya Kiuchumi nchini Malawi kuna haja ya kutafuta maeneo mapya na kuyaibua kwa kuongeza ushirikianao na kuweza kueleta tija kiuchumi kwa pande zote mbili.
Mhe. Othman ameyasema hayo leo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika Jamhuri ya Malawi Hampheray Polepole aliyefika ofisini kwa makamu Migombani mjini Zanzibar kujitambulisha.
Amesema nchi ya Tanzania inaweza kujifunza katika maeneo meingi yakiwemo ya kilimo na bishara kutoka nchini Malawi na kuibua vyanzo vipya vya biashara kati ya nchi hizo mbili na kuweza kuleta neema kubwa kwa Tanzania na Malawi kupitia ushirikiano wa diplomasia ya kiuchumi.
Mhe. Makamu amemueleza balozi Polepole kwamba suala hilo litawezekana iwapo Balozi huyo atazingatia ipasavyo sera ya nje yaTanzania ambayo inaongozwa na mfumo wa diplomasia ya kiuchumi inayohimiza masuala ya ushirikiano kwenye maeneo mbali mbali ya kimaendeleo.
Amesema upo uwezekano wa kutumia uzoefu wa Malawi kwenye mambo memgi ambayo nchi ya Malawi imefanya vyema na kufanikiwa na hivyo Tanzania ikaweza kunufaika na kuwepo uwakilishi wa Balozi huyo kwa kuongeza ushirikiano zaidi wa Kidplomasia kwenye maeneo mapya.
Aidha Mhe. Othman amesema kuwa kuna haja pia ya kutumia ushirikiano wa karibu kijamii na wa asili uliopo muda mrefu baina ya pande hizo mbili ulioanzia tokea harakati za ukombozi ili usaidie kuongeza nafasi ya ushirikiano kwenye maeneo tofauti.
Mhe Othman amemtaka Polepole kuhakikisha anatumumia , ujuzi maarifa na uwezo wake wote aliionao ili lengo la kuaminiwa na kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi ya Malawi liweze kutimia.
Alimuhakikisha Balozi hiyo kwamba Serikali ipo tayari wakati wote kutoa ushirikikiano unaohitajika wa kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeaza wakati wa kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya Tanzania.
Naye Balozi Pole Pole ameshukuru Makamu wa Rais na kuahidi kwamba atafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba anafanikisha malengo ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuomba na kupokea ushauri kutoka kwa viongozi mbali mbali pale itakapohitajika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...