MSANII wa muziki wa R&B Bernard Paul 'Ben Pol' amesema ameamua mbali na muziki ataendelea kutumia sauti na jina lake katika kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.

Pol amesema kuwa sasa anashiriki katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inayofanyika kila mwaka ambapo kwa kushirikiana na ubalozi wa ufaransa walifanya tamasha jijini Dar es salaam mwezi Disemba mwaka 2021.                       

Amesema,  licha ya kufanya tamasha hilo pamoja na kutoa wimbo uitwao “Usawa” washirikiana na Siti & The Band & Shika ndoto kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.

"Mimi ni Shujaa niliyeteuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kutoa hamasa juu ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
Ni Balozi wa mazingira kupitia wizara ya nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira,
Balozi wa Justdiggit taasisi ya Kimataifa yenye mlengo wa kuifanya afrika kuwa kijani kwa kutumia njia asilia kwa kushirikiana na Lead foundation 
Balozi wa WildAid inayoshughulika na uhifadhi wa wanyamapori na kupinga ujangili "amesema

Pol amesema, katika Shughuli za kijamii anafanya kazi kwa Karibu na Shirika la WWF ambapo hivi Karibuni wamefanya wimbo unaitwa Africa Song for nature 
Alichaguliwa kuwakilisha Afrika Mashabiki katika World Youth Forum 2022 jukwaa kubwa zaidi la vijana duniani linalofanyika kila mwaka Nchini Misri na kukutanisha vijana kujadili utatuzi wa masuala mbalimbali yanayoikumba dunia
 
Ameongeza kuwa siku chache zilizopita ameachia wimbo mpya unaitwa “Twa dance” nilioshirikiana na Dallah, wimbo umetayarishwa na Nusder, unapatikana katika mitandao yote ya muziki na media zote, na sasa niko jikoni kuandaa albamu mpya ninayotarajia kuizindua Septemba mwaka huu.                                                  

Pol amesema katika albamu hiyo itakayoshirikisha miamba ya muziki kutoka pembe zote za Afrika.                            


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...