Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimewataka watafiti wa masuala mbalimbali kutumia tafiti zao kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof Stephen Maluka wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Wiki ya utafiti na uvumbuzi inafanyika kwa mara saba ambapo ilianzishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2015 baada ya kuona umuhimu wa tafiti zinazofanywa na wanataaluma, wanafunzi wa shahada ya kwanza na ya pili kuleta tija kwa jamii.

Prof Maluka amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa wiki ya utafiti na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ilikua ni kuhakikisha tafiti zinazofanywa na wanataaluma na wanafunzi zinasaidia jamii na sio kuishia katika Majarida na vitabu.

“Wiki hii ya utafiti tunataka kuona tafiti zinaoneshwa na wanataaluma hawa zinaenda kuleta tija kwa jamii, na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kiliamua kuanzisha wiki hii mwaka 2015 baada ya kuona tafiti nyingi zinafanyika ila zimekuwa zinaisha kwenye majarida na vitabu na kutokusaidia jamii,”amesema Prof Maluka

“Kwa mwaka huu sisi kama DUCE tunaahidi kuzisaidia tafiti zinazofanywa kuingia katika soko la bidhaa pamoja na kuzilinda tafiti hizi ili zisiibiwe na watu wengi na kutumika,”

Aidha, Prof Maluka amewataka wanataaluma hususani wanafunzi kujifunza mambo mazuri yanayofanywa na watafiti wa Chuo hicho na kuweza kupata mawazo ya tafiti watakazokuja kuzifanya.

Ameongeza kuwa, katika wiki hii ya tafiti kutafuta na ushindani na washindi watakaofanya vizuri watapata nafasi y kushiriki Wiki ya tafiti Chuo Kikuu cha UDSM.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Lugha Prof Amani Msokelo amesema jumla ya watafiti 54 wamejitolea kuonesha tafiti zao kwa mwaka 2022 huku asilimia 85 ni wanataluma na asilimia 15 ni wanafunzi kutoka shule za Mazoezi za Chang’ombe.

Amesema kwa mwaka huu kauli mbiu ya Wiki ya Tatifi ni Tafiti na Uvumbuzi wenye Tija na chuo cha Duce kimeingia makubaliano na Vyuo kutoka Marekani na Denmark kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali.

Chuo cha Duce kimewataka wadau wengine wa maendeleo wa sekta ya elimu kuendelea kushiriki na kutoa mchango wao katika Wiki ya Utafiti na Uvumbuzi.

Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof Stephen Maluka akizungumza na watafiti, wanataaluma na wanafunzi wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Utafiti na Uvumbuzi kwa mwaka 2022 utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia April 20-22 uliofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof Stephen Maluka akitembelea mabanda ya maonesho ya Wiki utafiti na uvumbuzi 2022 baada ya kuzinduliwa leo Yenye kauli mbiu ya Tafiti na Uvumbuzi wenye Tija. Uzinduzi huo umefanyika April 20 Katika Chuo cha DUCE na unatarajia kumalizika Aprili 22 mwaka huu
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof Stephen Maluka akitembelea mabanda ya maonesho ya Wiki utafiti na uvumbuzi 2022 baada ya kuzinduliwa leo Yenye kauli mbiu ya Tafiti na Uvumbuzi wenye Tija. Uzinduzi huo umefanyika April 20 Katika Chuo cha DUCE na unatarajia kumalizika Aprili 22 mwaka huu
Picha ya Pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...