Na Amiri Kilagalila,Mufindi
ZAIDI ya ekari 20 za mashamba yenye mazao mbali mbali katika kijiji cha Kitasengwa kata ya Makungu wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,zimeharibiwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Victor Kwihava amesema madhara mengine ya mvua hiyo yaliyotokana na maporomoko ya maji kutoka mlima Udzungwa yaliyosomba sehemu ya udongo na kufukia vivuko viwili yamesababisha kukatika kwa mawasiliano ya kitongoji cha Mwenge ziliko huduma muhimu pamoja na vitongoji vya Muongozo na cha Matumaini.

“Kijiji cha Mwenge ndiko ziliko huduma muhimu kwa maana ya shule ya msingi pamoja na zahanati kwa hiyo toka asubuhi kukawa hakuna mawasiliano tena na jitihada tunazoendelea nazo sasa ni kuweka sawa miundombinu”alisema Victor Kwihava

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule amethibitisha juu ya athari zilizotokana na mvua hizo huku akibainisha kuwa kwa sasa kumekuwa na mvua kubwa katika maeneo ya wilaya hiyo.

“Ni kweli na juzi,jana hadi leo kulikuwa na mvua kubwa kwenye baadhi ya maeneo lakini haswa kwenye bonde hili la Mgololo ambayo ilisababisha mito kujaa maji”amesema Mtambule

Amesema miongoni mwa watu walioathirika na mvua hizo ni pamoja na watoto wa shule ambao imepelekea kukosa masomo siku ya leo.

“Tulichukua hatua kwa watoto wa shule kwasababu nimeambiwa kuna vivuko viwili vimeondolewa kwa hiyo tulizui ili wasije wakapata shida ya maji,lakini pia kuna nyumba kama ishirini ambazo ziko kwenye mkondo wa maji pia hao tumewaambia watoke waende kwenye maeneo ya milimani”alisema Mtambule

Aidha amesema hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu zaidi ya miundombinu na mashamba huku akitoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari yanapotokea majanga kama hayo licha ya kujali shughuli zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...