Na Fredy Mshiu
Hatimaye
wananchi wa mtaa wa Kombo kata ya Vingunguti wameanza kupata huduma ya
majisafi na salama baada ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira
Dar es salaam (DAWASA) kuanza zoezi la kuwaunganishia huduma ya maji
wakazi wa maeneo hayo.
Hii
imekuja mara baada ya mradi wa maji wa jamii uliokuwa unahudumia
wananchi hao kukabidhiwa chini ya uendeshaji wa DAWASA na wananchi
kuingiwa na hofu ya kutoendelea kupata huduma.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Vingunguti, ndugu William Kibeyo akizungumza katika
mkutano wa wananchi aliwaondoa hofu wananchi juu ya huduma huku
akiwaeleza kuwa mabadiliko hayo ya uendeshaji wa mradi yanatokana na
takwa la kisheria na mabadiliko ya sheria namba 5 ya mwaka 2019
inayoitaka DAWASA kuhudumia maeneo yote ya kihuduma na shughuli za
jumuiya na kamati kukabidhiwa kwenye Mamlaka.
"Nitake
kuwatoa hofu, Serikali hii inayotuhudumia ndio ilileta mabadiliko ya
uendeshaji wa kamati zetu za maji za mitaa na kata na sisi kama viongozi
wa Wananchi hatuna budi kusimamia sheria hizi ili zitekelezwe.
Tunawahakikishia huduma itaendelea kupatikana kwa ubora na viwango
sahihi "ameeleza ndugu Kibeyo.
Ndugu
Kibeyo ameongeza kuwa wananchi miundombinu ya maji ya kamati
iliyojengwa na shirika la maendeleo la Plan International itaunganishwa
katika mfumo wa maji wa DAWASA na wananchi wasioweza kumudu gharama za
kuunganisha huduma ya maji majumbani basi wataendelea kuhudumiwa kupitia
kizimba hicho kwa gharama iliyowekwa na EWURA.
"Gharama
iliyowekwa na EWURA kwa ndoo ya maji ya Lita 20 ni Tsh 50. Hii
itasaiida familia ambazo bado hazijajipanga vizuri kuomba huduma ya maji
katika nyumba zao" alimalizia Ndugu Kibeyo
Kwa
upande wake meneja wa mkoa wa kihuduma DAWASA Tabata, Mhandisi Boniface
Ole amewaeleza wananchi kuwa zoezi la kufunga mita kwa wananchi
waliositishiwa huduma kwa sababu ya kutojisajili DAWASA imeanza na leo
jumla ya wananchi 29 wameomba kusajiliwa na wameshafungiwa huduma.
"Utaratibu
wa Serikali ni lazima mtumiaji wa maji awe na dira inayoonyesha
matumizi yake, hapa wengi walikua hawana dira na kupelekea kutumia
huduma ya maji bila kulipia. Awali tulisitisha huduma na kuwasihi
wananchi wajitokeze ili wajisajili DAWASA na kutambulika ili wafungiwe
dira za Maji. Muitikio ni mzuri kwani kati ya wananchi 100
waliositishiwa huduma , tumeweza kuwarudishia wananchi 29 na zoezi
linaendelea"ameeleza Mhandisi Ole.
Mhandisi
Ole ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajajaza fomu wala kujisajili
DAWASA wajitokeze Ili wafungiwe dira za maji na kuendelea kupata huduma
kwa haraka.
Ndugu
Aisha Ramadhan, Mkazi wa mtaa wa Kombo amesema hofu iliyokuwepo awali
ni wasiwasi wa kutopata huduma baada ya mradi kukabidhiwa DAWASA. Ila
baada ya elimu sasa wapo tayari kutumia maji ya DAWASA kama
walivyoelekezwa.
"Sisi
Maji ya DAWASA tunayahitaji sana, kwa maelezo tuliyopewa hapa leo ile
hofu yetu imekwisha, tunawaomba DAWASA maji haya yaendelee kutoka na
yasikatike mara kwa mara na tuwahakikishie kuwa kila mkazi wa kwa kombo
hapa Vingungiti yupo tayari kutumia maji safi na salama DAWASA" ameeleza
ndugu Aisha.
Mabadiliko
ya uendeshaji wa kamati za maji zilizokuwa chini ya Halmsahauri
zimefanyika kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Maji namba 5 ya Mwaka 2019
ambapo miradi yote ya jamii itakabidhiwa katika Mamlaka za maji kwa
usimamizi na uendeshaji wenye tija.
Mpaka
sasa jumla ya miradi 295 iliyokuwa ya jamii/kamati za maji katika Jiji
la Dar es salaam imekabidhiwa chini ya DAWASA kwa usimamizi na
uendeshaji.
Meneja
wa mkoa wa kihuduma DAWASA Tabata, Mhandisi Boniface Ole akizungumza na
wananchi wakati wa zoezi la kuwaunganishia huduma ya maji mtaa wa Kombo
kata ya Vingunguti
Meneja
Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro akizungumza na wananchi wakati wa
zoezi la kuwaunganishia huduma ya maji mtaa wa Kombo kata ya Vingunguti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...