Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo amemuwakilisha Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Emilio Mwai Kibaki. Ibada ya kumuaga Hayati Mwai Kibaki imefanyika katika Uwanja wa Nyayo uliopo Nairobi nchini Kenya na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, wawakilishi wa taasisi za kitaifa na kimataifa pamoja na mabalozi, wananchi wa Kenya na nchi jirani wamehudhuria kuagwa kwa Hayati Mwai Kibaki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki wakati wa Ibada ya kuaga mwili huo iliofanyika katika Uwanja wa Nyayo Nairobi nchini Kenya leo tarehe 29 Aprili 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimfariji Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta mara baada ya kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki. Tarehe 29 Aprili 2022.
…………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo amemuwakilisha Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Emilio Mwai Kibaki. Ibada ya kumuaga Hayati Mwai Kibaki imefanyika katika Uwanja wa Nyayo uliopo Nairobi nchini Kenya na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Katika tukio hilo, Makamu wa Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara) Komredi Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk.
Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, wawakilishi wa taasisi za kitaifa na kimataifa pamoja na mabalozi, wananchi wa Kenya na nchi jirani wamehudhuria kuagwa kwa Hayati Mwai Kibaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...