NA PATRICIA KIMELEMETA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Ng'wilabuzi Ludigija amesema kuwa, wanafunzi wa madarasa ya awali wanakunywa uji wenye virutubisho Ili kuwapuesha na udumavu na utapiamlo jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma afya zao
Akizungumza Jana, Ludigija amesema kuwa, licha ya wanafunzi wa madarasa hayo kutumika muda mchache wa kukaa darasani,kujifunza kusoma na kuandika lakini pia kucheza, bila ya kuwa na afya bora hawataweza kushiriki kwenye vipindi hivyo.
AlIsema kuwa, licha ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali za wazazi kushindwa kuchangia lishe mashuleni, làkini Jiji hilo limeweza kutafuta wadau mbalimbali ambao wamejitokeza kufadhiri chakula katika baadhi ya shule, jambo ambalo limesaidia watoto kupenda kusoma.
"Baadhi ya shule zilizopo Mjini tumeweza kupata wafadhiri ambao wamekuwa wakichangia lishe mashuleni Kwa wanafunzi wa awali, lengo ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupenda kusoma, kukuza ubongo wao, pamoja na kuondoa udumavu na utapiamlo ambao unaweza kuwarudisha nyuma kiafya," alisema Ludigija.
Aliongeza kuwa,licha ya wanafunzi hao kukaa muda mfupi darasani, làkini pia wanapaswa kuwa na afya bora inayoweza kuwasaidia kujifunza na kukuza ubongo wao.
Alisema kuwa, Maofisa lishe wa Jiji hilo wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa, Watoto hao wanakunyawa uji wenye virutubisho vyote.
Naye Ofisa lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe(TFNC),Gelagister Gwalasa amesema kuwa, ili moto aweze kujifunza vizuri anahitaji kula vyakula bora vyenye virutubisho vyote ambavyo vitamsaidia kukuza afya ya Mili na akili.
Alisema kuwa, lakini pia,watoto shule za awali, wanapaswa kutengewa muda wa michezo ili kuimarisha afya zao.
" Watoto wa madarasa ya awali wanahitaji kula mlo kamili ambao una virutubisho vyote kwa akili ya kuwajenga kiafya ya akili na mwili, lakini pia kuwaepusha na magonjwa ambavyo yanaweza kuwarudisha nyuma," alisema Gwalasa.
Aliongeza kuwa, muda ambao wanakua shuleni, wanapaswa kunywa uji wenye virutubisho vyote ili waweze kuimarisha afya zao.
Hata hivyo, Mwalimu wa shule ya Awali, Amina Khamis anasema kuwa, licha ya watoto hao kuwa na muda mchache wa kujifunza, lakini wanawaa muda wa kucheza kwa ajili ya kuimarisha afya ya ubongo.
" Baada ya kumaliza kunywa uji, wanapumzika kidogo halafu tunawapa vifaa changamshi vya kujifunzia ili kuwapima ubongo wao unavyoweza kujifunza," amesema Amina.
Ameongeza kuwa, serikali imetoa mwongozo kwa shule zote za awali Ili ziweze kuwa na vifaa changamshi vya kujifunza, lakini pia kuwapa uji wenye lishe Ili kuimarisha afya zao.
Serikali ilizindua Mpango Jumuishi wa Taifa wa Malezi,makuzi na Maendeleo ya Awali ya moto(PJT-MMMAM) wa Mwaka 2021-26 ukiwa na lengo la kutatua changamoto za mahitaji kwa Watoto Ili kuondoa udumavu.
Kukosekana kwa uhakika wa chakula kunasababisha msingi wa mawazo, udumavu, utapiamlo na ubongo kutokuwa vizuri, hivyo basi mpango wa Malezi Jumuishi nchini unahitaji kupewa kipaumbele na kuratibiwa vema Kwa sababu tafiti zinaonyesha kuwa,Dola Moja ya Kimarekani inayowekezwa kwenye afua Jumuishi ya MMMAM inaweza kuzalisha dola za kimarekani 17.
Aidha ushahidi unaonyesha kwamba, uwekezaji katika elimu ya Awali,kwa watoto walio katika mazingira hatarishi unarudisha faida inayokadiriwa kuwa asilimia 7 hadi 16 kwa Mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...