WATANZANIA waasawa kutembelea katika maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yanayoendelea kuanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022 na Kesho Aprili 28,2022.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho hayo, Diwani wa kata ya Keko, Jasdeep Singh Babhra amewaalika watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani vyuo vya India vinawaalika kwenda kusoma katika nchi yao.
"Vyuo vya India vinafursa nyingi sio za elimu tuu hata fursa za michezo zipo kwa watu wenye vipaji vya michezo mbalimbali." Amesema Babhra
Kwa Upande wake Mbunge wa zamani na aliyekuwa Naibu Waziri kwenye Wizara mbalimbali nchini, Shamim Khan amewaasa watanzani kuchangamkia fursa hiyo na sio kwenda katika nchi ya India ikiwa hawajatangaza fursa za masomo kama hivi sasa.
Amesema kuwa Nchi ya India imetangaza uadhili wa masomo (scholarships) 500 kwa watanzania kwenda kusoma katika nchi hiyo.
Akishukuru serikali ya Tanzania na Serikali ya India Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Anorld Peter amesema kuwa wanafunzi walioenda katika maonesho hayo wachukue fomu kwaajili ya kujiunga na ani mbalimbali zilizotangazwa na India ili waende kujichotea maarifa ambayo yatasaidia Tanzania baadae.

Balozi wa India nchini, Binaya S.Pradhan akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.

Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Morogoro, Shamim Khan akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.

Picha ya pamoja wakati wa wa uzinduzi wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.
Picha ya pamoja wakati wa wa uzinduzi wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.
Balozi wa India nchini, Binaya S.Pradhan wa pili kutoka kulia akiwa katika Picha ya pamoja wakati wa wa uzinduzi wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.
Balozi wa India nchini, Binaya S.Pradhan akimsikiliza mmoja wa waelekezaji mara baada alipotembelea banda la moja ya chuo cha India katika Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.
Matukio mbalimbali wakati wa Maonesho ya vyuo Vikuu vya Nchini India yanayoanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Aprili 27,2022.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...