SERIKALI imepongeza kazi kubwa na mzuri inayofanywa na mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya uchimbaji wa madini chini ya ardhi bila kulazimisha kushuka chini kama inavyofanyika katika shughuli za uchimbaji katika migodi mingine nchini.

Teknolojia hii imevutia viongozi mbalimbali,Wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya madini wanaoendelea kutembelea banda la Bulyanhulu lililopo Maonesho ya Wiki ya Usalama Mahali pa Kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetin Center jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, alitoa pongezi kwa Barrick Bulyanhulu kwa kuwa mgodi wa kwanza nchini kuwa na mitambo ya kieletronikali ya kimataifa katika shughuli za uchimbaji wa madini sambamba na maabara ya kwanza ya kisasa ya kupima madini (Auto-Mining and crysos Photon Assay Laboratory)

Alisema Barrick Bulyanhulu, imefanya mapinduzi makubwa sana ya kidigitali ambayo yanawezesha shughuli za uchimbaji madini kuwa salama tofauti na uchimbaji usio wa matumizi ya teknolojia za kisasa.
Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra,akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa ujumbe wa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ulipotembelea banda la Barrick kwenye manesho ya OSHA jijini Dodoma.
.Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra,akitoa maelezo ya shughuli za Mgodi kwa Wananchi na wadau waliotembelea banda la maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Mh.Ridhiwan Kikwete,alipotembelea banda la maonesho la Barrick jijini Dodoma


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akiongea baada ya kutembelea banda la Maonesho la Barrick Bulyanhulu (Katikati) ni Afisa Afya Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Dk.Said Kudra na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Adelhelm Meru
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Mh.Ridhiwan Kikwete,alipotembelea banda la maonesho la Barrick jijini Dodoma
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Mh.Dkt. Adelhelm Meru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...