Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka wanafunzi wa Shule ya Msingi Zamzam iliyopo Dodoma Jiji kumtanguliza Mungu na kuweka jitihada katika masomo yao ili kuweza kufikia mafanikio ya kitaaluma na kidini na hivyo kutoa mchango wao katika ujenzi na ustawi wa Taifa Tanzania.
Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa hafla ya futari kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Zamzam ya Jijini Dodoma, hafla ambayo amekuwa akiwaandalia wanafunzi hao kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,katika shule hiyo asilimia kubwa ya wanafunzi ni watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Katika hafla hiyo ambayo aliongozana na Uongozi wa BAKWATA mkoa,Viongozi wa CCM Kata na Timu ya DODOMA JIJI,Mbunge Mavunde ameahidi kuchangia kilo 1000(tani moja) ya mchele,mafuta ya kula lita 300,jezi za watoto wa kiume na kike,pamoja na magoli ya Chuma kwa ajili ya uwanja wa Michezo uliopo shuleni.
Wakisoma Risala yao kwa Mbunge Mavunde,wanafunzi hao wameshukuru Mbunge Mavunde kwa moyo wake wa kuwajali kila mwaka kwa kushiriki nao futari na kumuomba aendelee kuwa nguzo katika kuwasaidia watoto wanaosoma Zamzam ili waweze kufikia malengo yao ya kimasomo.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...