Na Pamela Mollel,Arusha
Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jijini Arusha,Pendael Mollel{47} Mkazi wa Kir anyi Jijini Arusha jana amepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la Mauaji.
Mbali ya Mollel wengine aliounganishwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na Onesmo Laizer{35} mkazi wa Ngaramtoni wilayani Arumeru ambaye pia ni mlinzi wa Mfanyabiashara huyo na mtuhumiwa mwingine Deogratias Mollel{25} mkazi wa Sakina Jijini Arusha ambaye ni Mdogo wa Mfanyabiashara huyo.
Akisoma shitaka la Mauaji,Mwendesha Mashitaka waSerikali,Grace Medikenya mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha,Devotha Msofe ilidaiwa kuwa mtuhumiwa Mollel na wenzake wawili walimuua kwa kukusudia Stephen Kivuyo{43} katika tukio lililotokea aprill 18 mwaka huu katika eneo la Burka Jijini Arusha majira ya saa 1.45 usiku.
Baada ya kusomewa shitaka hilo Hakimu Msofe aliwaeleza watuhumiwa kuwa mahakama hiyo haina Mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo kwani kesi hiyo ya Mauaji itasikilizwa na Mahakama Kuu hivyo hawatakiwi kujibu chochote na kesi yao ilihairishwa hadi Mei 10 mwaka huu itakapokuja kutajwa tena.
Mollel alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi na akiwa mahakamani hapo alionekana kuwa mpole na mnyonge huku idadi ndogo ya ndugu na jamaa zake wakijitokeza mahakamani.
Marehemu Steven alizikwa nyumbani kwake Ilkiushin ,wilayani Arumeru,mkono hapa,April 26 mwaka huu, jumanne wiki hii na ameacha mjane mwenye ujauzito mkubwa na wanae watano wadogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...