Rais wa Jamhuri Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Wakuu wa Mikoa katika Halmashauri ambazo mfumo wa M-MAMA utatekelezwa, kutenga fedha zitakazoongeza nguvu kwenye huduma ya mama na mtoto mchanga.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) iliyoratibiwa na kampuni ya simu ya Vodacom katika viwanja vya Chinangali.

Rais Samia amesema lengo la mfumo huo ni kuhakikisha kuwa wakina mama zaidi ya milioni moja ambao ni walengwa wanafikiwa na kunufaika na huduma hii katika kipindi cha miaka mitano.

Aidha, Rais Samia amesema tangu kuanza kwa majaribio ya mfumo wa M-MAMA katika Wilaya ya Sengerema na mkoani Shinyanga mwaka 2013, wanawake na watoto 12,000 wameshahudumiwa na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya kina mama vinavyotokana na ukosefu wa usafiri.

Vile vile Rais Samia ameitaka kampuni ya Vodacom kuufanya mfumo huo uwe endelevu na uwafikie wananchi wengi na kutoa wito kwa kampuni zingine zilizopo nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Rais Samia amesema, pamoja na jitihada zilizofanywa na Serikali, bado zipo changamoto ambazo husababisha vifo vya mama na mtoto kabla au baada ya kujifungua kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya haraka na usafiri wa uhakika wa kumwahisha mama mjamzito kufika katika kituo cha afya.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kulinda taarifa binafsi za watumiaji wa M-MAMA ili zikusanywe, kuchakatwa na kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazokubalika kimataifa.


ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...