Kaimu meneja wa miradi TENMET, Alistidia Kamugisha akizungumza na waaadishi wa Habari hawapo (pichani) juu ya maadhimisho ya Juma la Elimu yatakayofanyika Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Igunga kuanzia tarehe 25 hadi 29 April 2022 Maadhimisho haya yataongozwa na kauli mbiu Tuwekeze katika Elimu, kwa Elimu Bora na ujumbe “Elimu Kwanza”.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZHYhMWkIlWwvPst21ernKP7EM0WXvzC9Qp2T5EIXRLjzj6sccE0O-nB9V9R5yWrhYuqpuUhyZvwWqDZxftidOw6S6a3RlRWFHo3TVS4HSCLOi10riJRcxdY2iZzfPM0rBqiXlgWu4QYld_OKD3RCwq38iJFMelpXaNKCP6qL2rm4X49k4qcU/w640-h426/WhatsApp%20Image%202022-04-19%20at%202.44.39%20PM.jpeg)
Dkt. Ellen Otaru Mwanachama wa TENMET (katikati), akizungumza na waaadishi wa Habari hawapo (pichani) juu ya maadhimisho ya Juma la Elimu yatakayofanyika Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Igunga kuanzia tarehe 25 hadi 29 April 2022 Maadhimisho haya yataongozwa na kauli mbiu Tuwekeze katika Elimu, kwa Elimu Bora na ujumbe “Elimu Kwanza”.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheecyElYy_YCunDEIX-30dUCOibBO5nD7qhNqd7m9Nn8ICccOJdUX4lVRiKBuCSRGAwbyjL6ujgSEJc0tYqqmIXdbBQvlLy__gHEHUDLkQXnkuA7hq0I1rlxaLPlg1sDnHtX06JIT71tzwtBH4DppoZ7ibTA8C72afThBC-MBe4ZF-NGPew-s/w640-h426/WhatsApp%20Image%202022-04-19%20at%202.44.35%20PM.jpeg)
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batlda Burian anatarajiwa kufungua Maadhimisho ya wiki ya Elimu Aprili 25, 2022 Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 19, 2022 jijini Dar es Salaam, Kaimu meneja wa miradi TENMET, Alistidia Kamugisha amesema kuwa Maadhimisho hayo yatafungwa na Waziri wa OR-TAMISEMI, Innocent Bashungwa Aprili 29, 2022 mkoani humo.
"Mkoa wa Tabora umechaguliwa kufanyiwa maadhimisho ya Juma la Elimu kwa lengo la kuungana na wenyeji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote."
"Tunatambua juhudi mbalimbali zinazoendelea mkoani huko kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa elimu bora kwa wote lakini si vibaya pia na TEN/MET kama mtandao wa elimu wa kitaifa kushirikiana pamoja nao ili kuongeza nguvu zaidi na kufikia malengo." Amesema Alistidia
Amesema Maadhimisho ya wiki ya Elimu yameendelea kuchechemua maendeleo ya elimu kwenye mikoa na wilaya husika ambazo yamekwisha fanyika.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wenye nia njema, wapenda elimu kuungana na TENMET pamoja na Serikali ya Mkoa wa Tabora, wilayani Igunga katika umaliziaji wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wa shule ya Msingi Igunga ili kuongeza ulinzi kwa watoto na kuboresha mazingira ya kujifunzia ili asiachwe yeyote nyuma katika kupata elimu.
Amesema ili kufanikisha tuma mchango wako kwa namba hizi: Vodacom 0743 001 393 au Tigo 0678 280 859 Tanzania Education Network.
Maadhimisho yatahusisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo; kutembelea baadhi ya shule, kuendesha mikutano na kushiriki kazi za maendeleo ya jamii hasa mashuleni, kutakuwa pia na kongamano la elimu kimkoa lenye lengo la kuangazia kwa mapana changamoto za kielimu mkoani hapo na namna ya kuzitatua.
Maadhimisho hayo yataongozwa na kauli mbiu “Tuwekeze katika Elimu, kwa Elimu Bora na ujumbe “Elimu Kwanza”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...