
Mkurugenzi Mkuu wa shirika SOS Children's Villages Tanzania David Mlongo akizungumza katika uzinduzi ulioboreshwa 2022-2026 Jijini Arusha


Mkuu wa Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ASP Happyness Temu akizungumza katika uzinduzi ulioboreshwa 2022-2026 Jijini Arusha





Baadhi ya washiriki kutoka katika Asasi za kiserikali na zime za kiraia wakiwa katika Uzi duzi ulifanyika hivi karibuni Jijini Arusha

Baadhi ya washiriki kutoka katika Asasi za kiserikali na zime za kiraia wakiwa katika Uzi duzi ulifanyika hivi karibuni Jijini Arusha

Mkuu wa wilaya ya Karatu ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akiweka Saini kwenye uzinduzi wa upanuzi wa mradi ulioboreshwa 2022-2026
Na Vero Ignatus,Arusha
Taasisi ya SOS Children's Village, hivi karibuni imezindua upanuzi mradi wa miaka 5 (2022-2026) ulioboreshwa, unaotekelezwa na shirika hilo Mkoani Arusha,unaolenga watoto walio katika mazingira hatarishi/magumu na wale waliokosa malezi.
Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo,David Mlongo alisema kuwa SOS Childrens Village Tanzania kwa ufadhili wa SOS Children's Village Norway, imeona umuhimu wa kupanua mradi wake huo kwa lengo la kuwafikia wahitaji zaidi.
Alisema kuwa mradi huo utazigusa halmashauri zote za Arusha,ambapo kwa sehemu ya awali ya utekelezaji utajikita zaidi hatika Halmashauri ya Jiji la Arusha,Wilaya ya Arusha,Meru na Karatu Lengo likiwa ni kuboresha maisha ya watoto vijana na familia katika mazingira hatarishi kwa kutumia mifumo ya Serikali iliyopo.
Aidha Mlongo ameushukuru Uongozi wa mkoa wa Arusha kwa kufanikisha upatikanaji wa sehemu za ofisi ,katika majengo ya halmashauri zitakazotumiwa na wafanyakazi wa shirika, katika kuhakikisha wanafikisha huduma kwa wananchi kwa ukaribu zaidi.
"Kila mtoto anastahili mahali bora na salama kwaajili ya kukua kwake mazingira rafiki ambapo nahitaji yake mengi yote yanapewa kipaumbe, na yaweze kutimiziwa.Niwaombe wadau wengine wajitokeze na kuongeza juhudi zao na kubuni miradi inayofanana na hiyo ,Kushirikiana kwa pamoja katika ulinzi wa mtoto na uwezeshaji wa familia" alisema Mlongo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wa shirika ya SOS Children Village Haruna Masebu alisema kuwa majukumu yao ni kusimamia ,kushauri kubuni mipango na kuhamasisha Maendeleo ya miradi mbalimbali ya shirika inayotekelezwa nchini, kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zao kwa kuzingatia dira ,shabaha ya Serikali na sera mbalimbali za Kitaifa na miongozo ya Kimaraifa
"Baadhi ya miongozo ya Kimataifa ni pamoja na Shirikisho la kimataifa la haki ya mtoto,Malengo ya kimataifa ya Maendeleo endelevu,miongozo ya Kimataifa ya malezi mbadala ya watoto Sera ya Kimaraifa ya kumlinda mtoto,Kitaifa sera ya ulinzi na ustawi wa mtoto,sheria ya mtoto ya 2009 pamoja na sera ya Maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008"alisema Masebu
Alisema zaidi ya miaka 30 Sasa shirika hilo la SOS Children Village limekuwa linatoa huduma ya malezi mbadala katika vituo vyake vya Zanzibar,Arusha ,Dar-es-salaam ambapo kwa muda wote shirika limeweza kushiriki kwa vitendo sera hizo.
Masebu amezitaja changomoto ambazo shirika linapitia ikiwa ni pamoja na wananchi kulichukulia kama chombo cha kutoa fedha ,na kupelekea upotoshaji wa malengo mahsusi ambayo ni kuwasaidia watoto ambao wanachangamoto ya malezi na waliofanyiwa vitendo ya Ukatili.
Kwa upande wake mgeni rasmi Dadi Horace Kolimba alilipongeza shirika hilo kwa usimamizi mzuri katika kuleta ustawi wa watoto kwa Maendeleo ya Taifa,kwani limekuwa likishirikiana na Serikali katika utekelezajiwa sera mbalimbali, zinazowezesha kutimiza Malengo ya kuwahudumia watoto na familia,katika mazingira hararishi mikoa ya Arusha,Mwanza,Dar-es-salaam,Iringa na Visiwa vya Zanzibar.
Aidha alisema kuwa changamoto zilizobainika 2020 ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji ya vijana,Elimu ya ufundi stadi,kukosekana kwa mifumo imara ya ulinzi wa mama na mtoto katika baadhi ya wilaya ,unyanyasaji wa watoto Pamoja na Jamii kutokuwa na ujuzi wa malezi mbadala zitathibitishwa zaidi katika zoezi la ukusanyaji wa takwimu za awali utakaofanyika 2022 kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi.
Kolimba alihitimisha kwa kusema kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa mradi huo utaongeza nguvu katika kuboresha uchumi wa familia vijana katika mkoa wa Arusha
Alisisitiza kuwa SOS imeona umuhimu wa kupanua mradi huo katika mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwafikia wahitaji zaidi ambapo halmashauri 4- zitanufaika na mradi huo Ila Mpango wao ifikapo 2024 mkoa mzima uwe umeingua katika mradi huo
Amesena kuwa Kuhakikisha wanahamasisha Jamii na mifumo yote ya familia ambazo zimekuwa na changamoto kuhakikisha watoto wanabakia kwenye familia na siyo kwenda kwenye makazi ya watoto ,kwani zipo changamoto nyingi wanazopitia watoto wanaolelewa nje ya familia
Familia zinajengewa uwezo wa kujimudu ili kuhakikisha wanapata nahitaji ya watoto
Mgeni rasmi aliyemuwakulisha mkuu wa mkoa wa Arusha Dad Kolimba Amesema kuwa ameipongeza shirika hilo kwa upanuzi wa mradi katika maeneo mengine ambayo yalikuwa hayana mradi ambapo ndani ya mikaa 10 ulikuwa aukitekelezwa katika Halmashauri ya Arusha pekee
Aidha amewashukuru kwa mradi huu kupanuliwa na kuingia katika Halmashauri nyingine tatu, katika kuleta malezi ya watoto kwa ustawi wa watoto wetu na Taifa kwa ujumla kwani limekuwa mdau mkubwa katika kuleta watoto waliopo katika mazingira hatarishi
Naupongeza Uongozi wa shirika kwa kubini mradi utakaoshirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu mabalimbali ufanisi na utekelezaji wa mradi huo utadaidia maeneo mengine utajifunza namna ya kutekeleza mradi huo.hivyo ili kufananiasha mradi huo Viongozi katika ngazi za mkoa na wilaya tulichukue na kuhakikisha linatendewa haki kwaajili ya kufikia kundi kubwa la watoto,vijana kwaajili ya kuleta Maendeleo zaidi kwa kuzingatia maarifa, ili ya kiutumishai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...