Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Munkinya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi katika  kata hiyo aliyoifanya jana ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na Wazazi na Walezi wa wanafunzi hao.
Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanafunzi hao.
Wazazi na Walezi wakiwa kwenye mkutano huo.
Afisa Elimu wa Kata ya Dung;unyi, Ester Mkoma (kushoto) akizungumza na Wazazi na Walezi katika ziara hiyo.
Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wazazi.
Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wanafunzi wa shule hiyo. 

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

AFISA Mtendaji wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku ametoa onyo kali kwa Wazazi na Walezi wenye tabia ya kuwarubuni watoto wao waache kwenda shuleni huku wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo ya kutaka kuwaoza. 

Njiku alitoa onyo hilo jana alipokuwa akizungumza na wazazi na wanafunzi  wakati wa ziara yake ya kukagua miradi katika Shule ya Sekondari Munkinya ilioyopo katika kata hiyo. 

" Hivi karibuni kumezuka tabia ya  baadhi ya wazazi kuwarubuni watoto wao waache shule ili wabaki nyumbani kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kuwaoza  na wengine wanaambatana na watoto wao mpaka ofisi za Serikali za Vijiji na kata ambako wamekuwa wakitoa madai eti watoto wao hawataki shule hivyo wanaomba wafutwe" alisema Njiku. 

Njiku alisema mzazi au mlezi atakaye bainika akifanya hivyo hatamvumilia atamkamata na kumfikisha kwenye vyombo cha dola na katika jambo hilo hata kuwa na huruma na mtu.

Alisema ni jambo la ajabu kwa mzazi na mlezi kufanya jambo hilo kwani Serikali imetumia fedha nyingi kuboresha miundombinu mashuleni ili watoto wapate elimu katika mazingira bora alafu anatokea mzazi akidai anataka mtoto wake aachishwe shule. 

" Itakuwa Serikali ya ajabu ambayo itaukubali upuuzi huo nasema ole wake  mzazi tukakaye mbaini akifanya hivyo" alisisitiza Njiku kwa ukali. 

 Alisema ni wajibu wa wazazi na walezi kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya elimu wawapo shuleni na nyumbani lakini si kwa kuwarubuni kuacha shule. 

Njiku alitumia nafasi hiyo kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia kiasi cha Sh. Milion 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule hiyo ambapo aliwasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...