NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bregedia Generali (BALOZI) Wilbert Ibuge amesema mwenge wa uhuru mkoani Ruvuma utapokelewa wilayani Nyasa tarehe 8 mwezi huu na ukiwa mkoani Ruvuma utakimbizwa umbali wa kilomita 1,052.3 katika Halmashauri zote 8 ndani ya wilaya 5 na kutatembelea miradi 62.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake Bregedia Generali Ibuge alidai Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Mwenge wa uhuru utakimbizwa siku ya tarehe 8 mwezi aprili katika umbali wa kilomita 161.1 ,huku Halmashauri ya wilaya ya Mbinga utakimbizwa siku ya tarehe 9 mwezi aprili umbali wa kilomita 106.5 na Halmashauri ya Mbinga Mji utakimbizwa umbali wa kilomita 72 siku ya tarehe 10 aprili.
Bregedia Generali Ibuge alizitaja Halmashauri zingine za wilaya ya Songea kuwa utakimbizwa umbali wa kilometa 94.3 siku ya tarehe 11 aprili na Halmashauri ya manispaa ya Songea utakimbizwa umbali wa kilomita 70.7 siku ya tarehe 12 aprili 2022, na Halmashauri ya wilaya ya Madaba utakimbizwa tarehe 13 aprili 2022 kwa umbali wa kilomita 247.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliwakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma kushiriki kikamilifu katika kuupokea na kuukimbiza mwenge wa uhuru ukiwa katika mkoa wa Ruvuma.
Mkoa wa Ruvuma utamaliza kukimbiza mbio za mwenge wa uhuru tarehe 15mwezi aprili 2022 baada ya kuukimbiza katika wilaya ya Namtumbo tarehe 14 mwezi aprili umbali wa kilomita 217 na Halmashauri ya wilaya ya Tunduru siku ya tarehe 15 mwezi aprili 2022 kwa kuukimbiza kilomita 83.7.
Aden Mbele mwandishi wa habari wa Radio Jogoo alimwuliza Mkuu wa mkoa wa Ruvuma kuhusu hali ya barabara ambazo zitatumika kuukimbiza mwenge wa uhuru kutokana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha hivi sasa na kuthibitishiwa kuwa barabara zote zinazoenda kutumika kupita mwenge wa uhuru zipo vizuri alisema mkuu wa mkoa huyo
Hata hivyo mwandishi wa habari Mawazo Mwaijengo wa AZAM alitaka kujua miradi iliyokataliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2021 na kutolewa maagizo ya kufanyiwa marekebishona nayo itakuwa katika ratiba ya kuipitia ili kujiridhisha na marekebisho yaliyoagizwa kufanyika aliulizwa mkuu wa mkoa ambapo alifafanua kuwa miradi yote iliyoagizwa kufanyiwa marekebisho na kiongozi wa mbio za mwenge 2021 ilifanyiwa marekebisho na tarifa za marekebisho ziliwasilishwa .
Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu 2022 umebeba ujumbe usemao “Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo ;shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya taifa”
Mwenge wa uhuru ukiwa mkoani Ruvuma utatembelea miradi 62 yenye thamani ya shilingi bilioni 5,202,463,637.66 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 29 yenye thamani ya shilingi bilioni 2,609,061,329.04 itafunguliwa ,miradi 5 yenye thamani ya shilingi bilioni 1,511,397,430.00 itawekewa jiwe la msingi na miradi 28 yenye thamani ya shilingi bilioni 1,082,004,878.00 kukaguliwa pamoja na kugawa vifaa mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...