Na Zuena Msuya, Lindi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua eneo la Likong’o litakalojengwa Mradi wa kusindika Gesi Asilia (LNG) na eneo la makutano ya kuunganisha gesi inayotoka mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi.
Akiwa katika ziara hiyo amewaasa watendaji wa maeneo hayo kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo ya kikazi, Mahimbali aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Kamishna Msaidizi wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Mohamed Fakih, na Meneja wa Kiwanda cha kuchata gesi asilia cha Madimba, Mhandisi Sultan Pwaga, pamoja na maafisa wengine kutoka wizarani na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Ziara hiyo imefanyika Aprili 2, 2022 mkoani Lindi.
Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara yake aliyoianza Machi 31, 2022 kwa kukagua mradi wa gesi wa Songosongo mkoani Lindi, kisha Aprili 1, 2022 alikagua kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, visima vya gesi katika eneo la Mnazi Bay pamoja mradi wa usambazaji wa miundombinu ya gesi asilia kwa matumizi ya kupikia majumbani.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (wa kwanza kushoto),
akitoa maelekezo kwa Watedaji wa Wizara hiyo na Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), alipowasili katika eneo litakalojengwa mradi wa
kusindika gesi asilia (LNG), Likong’o Mkoani Lindi
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) akionyeshwa
mchoro wa ramani ya eneo litakalojengwa mradi wa kusindika gesi asilia
(LNG), na Mjiolojia mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Simon Zabron, wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo
lililopo Likong’o Mkoani Lindi,
Kamishna
msaidizi wa Mafuta na Gesi wa Nishati nchini, Mhandisi Mohammed Fakih
akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri
Mahimbali (wa pili kulia), wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo lililopo
Likong’o Mkoani Lindi,
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, akikagua sehemu ya
mabomba ya gesi asilia katika kituo cha makutano ya kuunganisha gesi
hiyo inayotoka Mtwara na Songosongo Mkoani Lindi, mara baada ya
kutembelea kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha Somangafungu Mkoani
Lindi Aprili, 02, 2022.
Muonekano wa sasa wa eneo litakalojengwa mradi wa kusindika gesi asilia (LNG) lililopo Likong’o Mkoani Lindi, Aprili,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...