Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo leo Aprili 13,2022 amefunga mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo, Prof.Nombo amesema kuna umuhimu mkubwa kupitia mafunzo hayo yakatumike kwa vitendo na matokeo yake yaweze kuonekana.
Amesema kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo walimu hao ambayo yatawasaidia katika kuhakikisha ufundishaji na upimaji unafanyika vyema kwa wanafunzi ili wawe wataalamu wazuri kwenye masuala ya uhasibu na biashara nchini.
“Mafunzo haya yatatusaidia kuzalisha wataalamu ambao wataleta tija katika manufaa ya nchi yetu, ninaamini yatatusaidia sisi kama jamii kuweza kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”. Amesema Prof.Nombo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Anneth Komba amesema mafunzo hayo yameandaliwa na kuendeshwa na TET kwa ufadhili wa Serikali kupitia fedha za maendeleo zilizotolewa kwa taasisi hiyo katika mwaka wa fedha 2021/22 ambapo wamepokea kiasi cha Sh Bilioni 1.2.
Dk Komba amesema TET imelenga kushusha mafunzo hayo ngazi za chini kwa kuweka mazingira endelevu kwa walimu kazini katika ngazi ya Shule, Klasta na Vituo vya Mafunzo ya Walimu (TRCs) ambapo lengo hilo likifanikiwa kila Mwalimu atapata fursa ya kupata mafunzo mara kwa mara kwa gharama nafuu.
" Mafunzo haya yamehitimishwa leo ambapo walimu 451 wa masomo ya Book-keeping na Commerce kutoka Shule za Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali Tanzania Bara na Visiwani na kundi hili ni la kwanza yapo mengine yatafuatiwa. Naomba niwapongeze Washiriki wote wa kundi hili la kwanza.
Kundi la pili la Walimu 100 wa masomo ya ufundi watapata mafunzo haya katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga kwa muda wa siku sita kuanzia Aprili 20 hadi 25 na kundi la tatu litakua na walimu 400 wa masomo ya Uchumi na Kilimo na mafunzo hayo yatafanyika katika Chuo Cha Ualimu Morogoro kwa muda wa siku sita kuanzia Mei 1 hadi sita mwaka huu," Amesema Dk Komba.
Dk Komba amesema lengo kuu la mafunzo hayo kwa makundi yote matatu ni kuwajengea walimu uwezo wa kufundisha masomo ya michepuo kwa ufanisi mkubwa zaidi.
" Katika mafunzo haya Washiriki walifanya uchambuzi wa mihutasari ya masomo ya biashara ili kubaini mahiri wanazotakiwa kuwajengea wanafunzi, kutumia mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zinazozingatia ujenzi wa umahiri kwa wanafunzi.
Kuandaa shughuli za ujifunzaji na ufundishaji darasani, kufanya maandalizi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuandaa azimio la somo, andalio la somo na zana za ujifunzaji pamoja na kufanya ufundishaji kiduchu kwa kutumia andalio la somo waliloandaa kwa kuzingatia utumiaji wa mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji," Amesema Dk Komba.Mgeni
rasmi,Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
(WyEST) Prof.Carolyne Nombo akiwa akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba wakiagana na walimu wa
masomo ya Book Keeping na Commerce mara baada ya kufunga mafunzo ya
walimu Kazini kwa walimu wa masomo hayo,yaliyofanyika kwa siku sita
katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo
mkoani Pwani.
Naibu
katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST)
Prof.Carolyne Nombo akizungumza wakati akifunga mafunzo ya walimu Kazini
kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku
sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani
Bagamoyo. PICHA NA MICHUZI JR-MMG
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akizungumza
wakati wa ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya
Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha
Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo. Walimu
wa masomo ya Book Keeping na Commerce wakiwa katika ufungaji wa mafunzo
ya walimu Kazini kwa walimu hao yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo
cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.
Sehemu
ya Meza kuu ikifurahia jambo wakati Mgeni rasmi alipokuwa akimaliza
kusoma hotuba yake ya kufunga mafunzo ya Waziu kazini Bagamoyo mkoani
Pwani leo.Makofi yakipigwa mara baada ya kuisikia hotuba ya Mgeni rasmi
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo akiwa pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba
wakipata picha ya pamoja na walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce
wakati wa ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo
hayo,yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa
Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.PICHA NA MICHUZI JR-MMG
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...