Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema NBC inaendelea kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya kupitia ibada ya iftari.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya Iftar kwa wateja wa NBC wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sabi amesema benki ya NBC imeamua kufanya tukio hili kwa ajili ya kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya.
Sabi amesema, “tunamuni kufunga ni mafunzo, yanaleta maisha ya ukarimu, uchamungu, ukweli, furaha na mshikamano baina ya jamii,”
“Tunawashukuru wateja wetu kwa kuitikia wito na kuwa pamoja nasi katika hafla hii muhimu ya Iftar kwa ajili ya kurudisha kwa mwenyezi mungu kupitia ibada ya upendo, kutoa zaka na sadaka,”amesema
Aidha, Sabi ameendelea kuhamasisha watu binafsi na taasisi kuendelea kuwasaidia watu wengine kupitia ibada mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi akizungumza na wateja wa benki hiyo wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla ya Iftari iliyofanyika jana Katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi akimkabidhi Mswala Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakati wa hafla ya Iftari kwa ajili ya wateja wa benki ya NBC iliyofanyika jana Katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi akimkabidhi Mswala Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakati wa hafla ya Iftari kwa ajili ya wateja wa benki ya NBC iliyofanyika jana Katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza na wateja wa Benki ya NBC wakati wa hafla maalumu ya Iftari iliyofanyika Jana katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru (katikati) akijaliana jambo na wateja wa benki hiyo waliofika katika hafla ya Iftari kwa wateja wao iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa salum, wageni waalikwa na watendaji wa Benki ya NBC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...