BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema itaendelea kusapoti masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo sekta y afya hususani kwa magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Hazina, Masoko na Fedha Peter Nalitolela wakati wa mbio zijulikanazo kama Run 4 Autism zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Nalitolela amesema, benki ya NBC imeshiriki mbio hizo kwa sababu imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya na inajali afya ya Mtanzania ambapo watoto wenye autism (usonji) wanahitaji msaada pamoja na mengine ambayo yanaendana na hiyo.

Amesema, NBC imeshirikiana na Lukiza Foundation ambapo pia wameweza kuwalipia wakimbiaji ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo.

“NBC tunajali afya ya watanzania wote, afya ya mwili na akili na pia tunashirikiana na taasisi mbalimbali katika magonjwa yasiyotambulika au kupewa kipaumbele na ukiangalia kauli mbiu ya mwaka huu kuhusu autism (usonji) ni Elimu Jumuishi,”

“Elimu jumuishi inahusu kuwaweka watoto hawa katika mazingira mazuri ya kujifunza kwa ajili ya Taifa la kesho na pia kushiriki kwenye uzalishaji,”amesema Nalitolela

Naye Mzazi wa Mtoto mwenye Autism(usonji) Zaituni Simba ameziomba taasisi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia watoto hao ambao wamesahaulika na zaidi wanahitaji msaada kutoka kwao.

Zaituni amesema, amefurahi kushiriki mbio hizi leo kwa ajili ya watoto wetu wenye Autism (usonji), na anaamini yapo mataasisi mengine yatajitokeza kwa ajili ya kusapoti kuwasaidia watoto wao.

“Nawaomba watu wenye uwezo, watusaidie wasidhamini mambo mengine tu bali hata watoto hawa wanahitaji msaada wao na muda mwingine mzazi anashindwa kutoka au kwenda na mtoto sehemu kutokana na kushindwa kutembea,”amesema

Benki ya NBC imeshiriki mbio hizo kwa wafanyakazi wake kukimbia pia Julai 31 wanatarajia kuwa na NBC Marathon wanaamini washiriki walioweza kukimbia kwenye Run 4Autism watashiriki tena.
Wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) 


Wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio zilizoandaliwa na Lukiza Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wenye Usonji “Run 4 Autism” na kushirikisha taasisi mbalimbali, Mbio hizo zimefanyika mwishoni kwa wiki hii


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...