NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepewa Tuzo ya Kutoa
Huduma Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya
Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28,
2022 kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Aliyekabidhi
Tuzo hiyo ni Mgeni Rasmi katika sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce
Lazaro Ndalichako na ilipokelewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu, PSSSF, Paul Kijazi.
Siku
ya usalama na afya mahali pa kazi Duniani ni siku ya Kimataifa ya
kufanya kampeni ya kuboresha usalama na afya ya wafanyakazi, lengo ni
kuondoa hali zote hatarishi mahali pa kazi na hivyo kuifanya kazi iwe ya
hadhi na heshima na hufanyika kila mwaka kuelekea Siku ya Wafanyakazi
Duniani yaani Mei Mosi.
Kwa
mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi alisema ushiriki
wa Mfuko kwenye maonesho hayo ilikuwa ni fursa nzuri ya kukutana na
wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla ambao walifaidika kwa kupata
elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mfuko.
Alisema
wote waliofika kwenye banda la PSSSF walikutana na wahudumu wa Mfuko
ambao kazi yao kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapokea wageni kwa bashasha na
kutoa elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko, namna ya kupata taarifa
za michango kwa njia ya mtandao, jinsi ya mwanachama kuhakiki taarifa
zake
“Majukumu
ya msingi ya Mfuko ni pamoja na Kuandikisha Wanachama, Kukusanya
Michango, Kulipa Mafao lakini pia Kuwekeza kwa njia ya hisa kwenye
mabenki na kwenye maeneo mengine kwa mujibu wa sharia” alisema na
kuongeza……….Safari hii tumeshirikiana na Kampuni yetu tanzu ya
Kilimanjaro International Leather Industries Co. Limited (KLICL)
inayojisughulisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama vile viatu,
mikanda na mapochi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ((Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (wapili kushoto), akimkabidhi tuzo ya
Kutoa Huduma Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya
Usalama na Afya Mahali pa kazi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Paul
Kijazi wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28, 2022 kwenye viwanja vya Kituo
cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Katibu
Mkuu wa TUCTA Bw. Henry Mgunda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi na waanyakazi wa PSSSF kwenye banda la Mfuko huo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ((Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (wapili kulia mstari wa mbele), Naibu
Waziri Mhe. Ummy Nderiananga (wanne kulia) wakiwa kwenye picha ya
pamoja na viongozi na wafanyakazi wa PSSSF
Afisa
Uhusiano Mkuu, PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto) akimuangalia Msanii
maarufu nchini Mrisho Mpoto wakati akijipima kiatu cha kampuni ya KLICL
kinachomilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Magereza alipotembelea kwenye
banda la Mfuko huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu PSSSF, Bw. Ansigar Mushi (katikati) akimuhudumia mwananchi huyu kulia aliyetembelea banda la PSSSF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...