Na Vero Ignatus,Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatazamia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Royal Tour itakayofanyika kesho tar 28/4/2022 katika ukumbi wa Kimataifa AICC Mkoani Arusha

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kwa niaba ya kamati ya maandalizi amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Mhe.Rais anzia uwanja wa ndege wa KIA Hadi atakapoingia Jijini

Mongela amesema akuwa katika uzinduzi huo wanatazamia kupokea wageni zaidi ya 5000 kutoka sehemu mbalimbali na amesema kuwa ulinzi umeimarishwa vya kutosha hivyo kila atakayeingia atatoka salama bila shaka yeyote.

"Tunatazamia kuwa na ugeni mkubwa akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Spika wa Bunge,Visiwa vya Zanzibar,pamoja na wananchi wote wa mkoa wa Arusha maana shughuli hii inawahusu" alisema Mongela

Mongela amesema kuwa tukio hilo la uzinduzi mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan mwaka Jana alitumia muda mwingi katika kuandaa filamu hiyo nia na dhumuni kubwa ni kuhamasisha utalii katika Taifa la Tanzania.

"Kama wote tujuavyo filamu hii ya. The Royal tour yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa Kama mhusika mkuu Kama mwongoza utalii namba moja ambayo dhana kubwa kuendelea kutia chachu katika kuhamasisha utalii na kuleta tija kwa wananchi wote tuanakumbuka mwaka Jana alitumia muda mwingi na nguvu nyingi bila kuchoka kutengeneza filamu hii

Mongela amesema kuwa tar 18)4uzinduzi umefanyika new york Marekani, 21/4 ikazinduliwa nchini Los Angeles,28/4 utafanyika uzinduzi wa kwanza nchini Mkoani Arusha,baadae 7/5 Zanzibar na 8/5 Dar es salaam

Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo alisema kuwa wageni wote wasiwe na hofu ulinzi umeimarishwa

Aidha Masejo amesema kutokana na tukio la Kitaifa hivyo Jeshi la Polisi nchini kwa Kushirikiana na Kamati ya Usalama mkoa imehakikisha kuwa hali ni shwari na kila raia anakuwa salama.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...