Na Said Mwishehe, Michuzi TV-arusha
SERIKALI ya Mkoa wa Arusha imesema kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani ya CCM unaofanywa na viongozi wa Chama hicho umewezesha kupatikana kwa maendeleo katika mkoa huo.
Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Mkoa huo John Mongella amesema wamepiga hatua katika kila sekta na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan wameendelea kupata mabilioni ya fedha kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hiyo inatokana na uimara wa Chama hiki katika kusimamia Ilani.Tumepiga hatua kubwa kwa kila sekta.
“Katika sekta ya elimu yametokea mapinduzi makubwa, shule za msingi 14, sekondari 17 zimejengwa na ufaulu umeongezeka kwa watoto na mkoa wetu umeendelea kuwa moja ya mkoa ilioko kwenye tano bora kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
“Serikali imeendeela kutoa fedha ya elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari lakini tumeendelea kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu.Mapato yameongezeka ambapo kupitia mapato ya ndani Sh.bilioni 31zimepelekwa katika elimu.
“Tumepokea fedha za UVIKO-19 ambazo zimetumika kuboresha elimu ikiwa pamoja na kujenga shule shikizi.Kuna fedha za ruzuku za tozo Sh. bilioni 4.7 ambazo zimekwenda maeneo mbalimbali.Pia zaidi ya vituo 25 vya kutolea huduma za afya vimejengwa,”amesema Mongela.
Kuhusu maji amesema kuna miradi mbalimbali utekelezaji wa miradi ya maji unaendelea ambapo kuna vijiji 304 vina miradi hiyo na ifikapo mwaka 2025 watakuwa wamefikia vijiiji vyote kwa huduma ya maji na kwa Jiji la Arusha kupita mradi mkubwa wa maji hadi mwishoni mwa mwaka huu watapata maji kwa asilimia 100.
“Kazi hii yote ambayo inafanyika inatokana na uimaraza wa CCM katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani .Kila sekta kuna mafanikio makubwa, hata katika miundombinu ya barabara kuna kazi kubwa imefanyika.”
Aidha amesema Mkoa wa Arusha uko salama na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndio wenye duka na walioko Serikali wao ni wauza duka tu.”Watendaji wa Serikali wanajitambua na watasimamia Ilani ili kuendelea kuleta maendeleo.”
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Ndugu Abdulrahman Kinana,pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ndugu Zelothe Stephen wakisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM iliokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe,John Mongella kwenye mkutano wa ndani unaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mount Meru jijini humo.PICHA NA MICHUZI JR-MMG
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...