Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, alhaji Abubakar Kunenge ameuagiza uongozi wa Chama
kikuu Cha Ushirika Mkoani Pwani CORECU kuwachukulia hatua Kali za
kisheria wale watakaobainika kuhujumu Chama hicho.
Sambamba
na Hilo, ameupongeza uongozi wa mpito wa Chama hicho Kwa kusimamia
zao la korosho ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka Tani 7 mwaka
2019/20 Hadi kufikia Tani 15 msimu wa mwaka 2021/22 na Daraja la
kwanza la korosho kufikia Tani 72 ya Korosho zote.
Aliyaelekeza
hayo, katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama hicho
uliofanyika mjini Kibaha April 21,2022 katika ukumbi wa Shirika la Elimu
Kibaha.
Kunenge
alikitaka Chama hicho kiwe na utaratibu wa kuwajibishana endapo
kiongozi ama Mwanachama anaenda kinyume na taratibu za Chama hicho.
Pia amewataka wakuu wa Wilaya kuwachukulia hatua ,wanaoenda kinyume bila kujali itikadi za Chama.
Katika hatua nyingine RC Kunenge Amesema mkoa na Wilaya umedhamiria kuleta mapinduzi katika Zao la Korosho.
"Tumedhamiria
kuleta Mabadiliko katika Zao hilo la korosho ila peke yetu hatuwezi ni
lazima tushirikiane katika hili."alifafanua.
Vilevile
aliwataka Wanachama wa CORECU wasifanye makosa katika kuchagua viongozi
wapya baada ya uongozi wa mpito kumaliza muda wake.
Alisema
endapo Chama hicho kikipata viongozi waadillifu ,wasimamizi Wazuri na
watakaotosha Basi kitafanya vizuri katika majukumu yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...