Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Katika kuadhimisha Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoa wa Pwani umetoa misaada ya vitu mbalimbali na vyakula katika vituo vya kulelea watoto Cha Moyo Mmoja na kituo Cha Passion Kamelot children Home vilivyopo Bagamoyo.

Akikabidhi misaada hiyo, Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema , watoto hao Wana haki sawa na wengine hivyo katika kutambua Hilo ametoa vyakula na kujumuika nao pamoja .

Amesema kutoa msaada ni njia ambayo Ina tija kwa maana nae ni moja ya walezi.

Kunenge alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuwasemea watoto wanaoishi Mazingira magumu na Kuwa msaada kwao kwenye elimu na kujenga Mazingira bora ya jamii,jinsia , watoto,wazee na wenye ulemavu ili kila mmoja aishi kwa furaha.

Misaada iliyotolewa Ni Pamoja na Mchele,sukari,mafuta ya kupikia, maharage,vinywaji na mbuzi kwaajili ya kitoweo.

Aidha Kunenge akatumia muda huo pia kuwakumbusha Wananchi kushiriki zoezi la anuni za makazi na sensa ya watu na makazi Ili kurahisisha maendeleo kimkoa na Taifa kijumla.

Watoto na viongozi wa vituo hivyo Apaisara Minja ambae ni meneja Kituo Cha Moyo Mmoja na Sister Asteria Pantareo mlezi wa kituo Cha passion Kamelot 

children Home walishukuru kupatiwa msaada huo hasa nyakati hizi za sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...