- Ujenzi upo Asilimia 13 na Mkandarasi yupo mbele siku 15.

- Ameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kuidhinisha fedha Bilioni 26 kukarabati na kujenga soko la kariakoo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya maboresho na ujenzi wa Soko jipya Kariakoo linalogjarimu kiasi Cha Shilingi Bilioni 26 ambapo ameonyesha kuridhishwa na Kasi ya Mkandarasi na kumuhimiza kuhakikisha Ujenzi unakamilika kwa wakati.

RC Makalla amesema Mpaka Sasa Mkandarasi ameanza na mwendo mzuri na anaamini Kama ataendelea na Kasi hiyohiyo ni wazi Ujenzi utakamilika ndani ya Muda wa mkataba ambao ni miezi 18.

Aidha RC Makalla amesema kukamilika kwa Soko Hilo kutawezesha Soko kupokea idadi kubwa ya Wafanyabiashara tofauti na ilivyokuwa awali ambapo amesema kipaombele Cha kwanza kitatolewa kwa Wafanyabiashara waliokuwepo awali.

Hata hivyo RC Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kukarabati na kuboresha Soko la Kariakoo ambapo ameeleza pia Mkoa unatekeleza maelekezo ya Rais alieagiza kila Halmashauri kuboresha mazingira walipohamishiwa Wafanyabiashara pamoja na ujenzi wa masoko ya Machinga.

Kuhusu Ujenzi wa Soko la Jangwani, RC Makalla amesema tayari design ya Soko imekamilika na kinachosubiriwa kwa Sasa ni maamuzi ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Ujenzi.

Pamoja na hayo RC Makalla amepokea kero ya Mkandarasi wa Soko la Kariakoo ambae amekiri kukabiliwa na changamoto ya Wafanyabiashara kupanga bidhaa kwenye Barabara za kuingia kwenye eneo la Ujenzi na kusababisha adha kwa magari na mitambo ambapo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku Ufanyaji biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.

Ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo unatekelezwa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Estim kwa gharama ya Shilingi Bilioni 26 ambapo kwa mujibu wa mkataba kazi inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 18.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...