*Utoaji huduma, ukusanyaji wa michango, matumizi ya TEHAMA, ukwasi wa Mfuko yapewa kipaumbele
*Yajayo ni neema tupu NSSF kuvutia wanachama wapya kutoka makundi mbalimbali ya sekta isiyo rasmi
Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Balozi Ali Idi Siwa, amesema Mfuko utaendelea kusimamia maono ya
Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Watanzania waliopo kwenye sekta
binafsi na sekta isiyo rasmi wanasajiliwa na NSSF pamoja na waajiri
kuwasilisha michango stahiki ya wafanyakazi wao.
Balozi Siwa
alisema hayo jana jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 49 wa
Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, ambapo aliwataka watumishi wa Mfuko
kuendelea kutoa huduma bora, kujielekeza katika matumizi ya TEHAMA,
kushirikiana sehemu za kazi na kuifika sekta isiyo rasmi kwani imebeba
sehemu kubwa ya Watanzania ambapo kupitia kundi hilo Mfuko utapata
wanachama wengi wapya.
Alisema mpango wa mwaka na bajeti
pendekezwa ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2022/23, Mfuko umeweka malengo
mbalimbali ikiwemo kusajili wanachama wapya 313,478, kukusanya michango
ya shilingi trilioni 1.61 pamoja na kukusanya shilingi bilioni 383.5
ambazo ni mapato yatokanayo na uwekezaji.
Aliwataka wajumbe wa
baraza hilo wakawe kioo kwa wenzao ili Mfuko uweze kuwa na matokeo
chanya kwa wanachama na Mfuko kwa ujumla.
Naye, Ibrahim Maftah
ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, alisema Mfuko umefanya vizuri
katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni kuandikisha wanachama,
ukusanyaji wa michango, kuwekeza na kulipa mafao.
Alisema Mfuko
umefanya mapitio ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ili kuvutia wanachama
wapya kutoka katika makundi mbalimbali ya sekta isiyo rasmi ikijumuisha
wakulima, wavuvi, wamachinga, mama lishe, waendesha boda boda na bajaji.
"Lengo la mapitio hayo ni kuongeza wigo wa wanachama na kuwa na mafao yanayokidhi mahitaji ya makundi hayo," alisema Maftah.
Maftah
alisema katika mwaka wa fedha wa 2022/23, Mfuko unategemea ongezeko la
wastaafu 30,084 kutoka wastaafu 20,894 mwishoni mwa mwaka 2021/2022
Awali,
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Ekwabi Mujungu, alisema
watumishi wako tayari kuendelea kutoa huduma kwa mujibu wa taratibu
zilizopo.
Kwa upande wake, Willy Kibona ambaye ni Mkuu wa Sekta
ya Fedha TUICO Taifa alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kuishauri
Menejimenti kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kupitia mpango wa mwaka na
bajeti ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2022/23 pamoja na makadirio ya mapato
na matumizi.
"Tunashukuru kwa somo tosha kutoka kwa mgeni rasmi
ambalo litaweza kusaidia kujadili kushauri na hatimaye yale
yatakayokuwa tumependekeza tutakapokuja kwako kwenye Bodi yapate
baraka," alisema Kibona.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Balozi Ali Idi Siwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha 49 cha
Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, ambapo alisisitiza, matumizi ya
TEHAMA katika utendaji kazi, uboreshaji wa Huduma bora kwa wanachama na
kuendelea kuifikia sekta binafsi na sekta isiyo rasmi
Kaimu
Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ibrahim
Maftah, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.Akitoa maelezo ya
awali katika kikao cha 49 cha baraza kuu la wafanyakazi kilichofanyka
jijini Mwanza
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akiratibu ufunguzi wa
Kikao cha 49 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, kilichofanyika
Jijini Mwanza mwanzoni mwa wiki
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala NSSF Ekwabi Mujungu akitoa
salamu wakati wa Kikao 49 cha Baraza kuu la wafanyakazi wa NSSF ambapo
amesisitiza kuhusu kuendelea kusimamia vizuri maslahi ya wafanyakazi
na wafanyakazi kufanya kazi kwa mujibu wa miiko ya kazi ya utumishi wa
Umma
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akitoa neno la ukaribisho
wakati wa Kikao cha 49 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF
Mkuu
wa Sekta ya Fedha TUICO Taifa, Willy Kibona akitoa neno la Shukurani
kwa niaba ya wajumbe wa kikao cha 49 cha Baraza kuu la wafanyakazi wa
NSSF ambapo alieleza jinsi ambavyo Mabaraza yapo kisheria kwa madhumuni
ya kutoa ushauri na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi
Wajumbe wa Kikao cha 49 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, wakifuatilia Kikao.
Matukio katika picha wakati wa Kikao cha 49 cha Baraza kuu la wafanyakazi wa NSSF kilichofanyika jijini Mwanza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...