Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amewapongeza wakala wa barabara za Vijijini na mijini (TARURA) kwa ujenzi wa barabara zinapopita kwenye Mji wa madini unaojengwa Tanzanite City Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.
Makongoro akizungumza wakati akikagua barabara hizo amesema TARURA wamefanya kazi yao ipasavyo na thamani ya fedha iliyotumika Kwa ujenzi inalingana na ubora wa barabara.
Amesema wamezunguka kwenye barabara zinazojengwa na TARURA na kubaini ubora uliotumika hivyo wanastahili pongezi.
"Mmefanya kazi nzuri na hata Rais Samia Suluhu Hassan alisema mtu atakayefuja fedha ataona rangi yake halisi hapa hawezi kuwachukulia hatua ila atawapongeza," amesema Makongoro.
Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Manyara, mhandisi Meleck Slaa amesema ujenzi wa barabara za Tanzanite City umekuwa na changamoto mbalimbali kwani walitoa taarifa kwenye taasisi nyingine kuwa barabara itajengwa kwa upana wa mita 15.
"Kiuhalisia ilipaswa kuwa mita 25 na tukapata changamoto kwenye taasisi nyingine za TANESCO na maji kuhusiana na nafasi ya ujenzi wa barabara hizi za Tanzanite City," amesema mhandisi Slaa.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Paul Mabaya amesema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za maombi maalum.
Mhandisi Mabaya amesema barabara hizo za mradi wa Tanzanite City zinajengwa kwa kiwango cha moramu na ujenzi unaendelea.
Diwani wa kata ya Endiamtu, Lucas Chimba Zacharia amesema hatua ya ukamilishaji wa mradi huo utakuwa faraja kwa wananchi kwani kila mara wana shauku ya kutaka kufahamu hatima yake.
"Ninawapongeza viongozi wetu RC na DC wetu Dk Suleiman Serera kwa kuendelea kufuatilia mradi huu ili uweze kuke" amesema Luka.
Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian Laizer amesema wananchi watakuwa na imani na Serikali pindi mradi huo ukikamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...