Sera za usimamizi zinapaswa kuwa chachu wala sio kikwazo cha ubunifu
Tumefanya uamuzi mgumu wa kusitisha huduma zetu nchini Tanzania kuanzia Alhamisi ya Tarehe 14 Aprili 2022. Nauli elekezi iliyowekwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesababisha changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendelea kutoa huduma kwa wateja wetu. Inakua ngumu kwetu kuendelea kutoa huduma.
Hatuta weza kutoa huduma mpaka pale mazingira yatakapokua rafiki kwa sisi kuendelea kutoa huduma.
Tuweke Wazi: Tungependa sana kuendelea kutoa huduma zetu nchini Tanzania
Lakini, maandalizi ni sehemu muhimu katika kufikia malengo ya siku za usoni.
Siku zote, lengo letu ni kuwa mshirika muhimu katika miji mbalimbali kwa kutoa usafiri wenye ufanisi, kutengeneza fursa za kiuchumi zinazowapa madereva uhuru wa kujiingizia kipato kwa muda wanaotaka wao na kuchangia katika mapato ya serikali. Na tumelisimamia lengo hili tangu tulipofungua milango yetu katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2016.
Kipaumbele Chetu: kuwasaidia Madereva Watanzania
Uamuzi huu umekuja baada ya mamlaka kuweka kanuni ambazo ni changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendesha biashara yake. Tutafanya kazi kwa karibu na madereva kwenye mpito huu.
Tutarudi kuzindua huduma zetu mara tu kutakapokuwa na kanuni mpya.
Ingawa tumefunga huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika katika kuunda kanuni ambazo zitawezesha teknolojia kunawiri, ili tuanze tena kutoa huduma zetu zinazopendwa na watu wengu.
Asante, Tanzania!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...