Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge,ameingilia kati mgogoro wa ardhi
baina ya wananchi wavamizi pamoja na moja ya familia ambayo ndio
wamiliki halali wa eneo huko Kitongoji Cha Sanzale Kata ya Magomeni,
Bagamoyo.
Akiwa katika
eneo lenye mgogoro aliwataka wananchi hao, kuhakikisha wanalipa fidia
ya eneo hilo kwa kufuata makubaliano yaliyotolewa na familia.
Aidha
, amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Zainabu Abdallah kuhakikisha
anaendesha msako wa kuwakamata matapeli wote waliohusika katika eneo
hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria
"Naishukuru
familia ya marehemu kwa kugoma kubomoa nyumba za wananchi hawa
,Namuagiza Mkuu wa Wilaya kufuatilia kwa karibu ili wakishakubaliana
watu hawa wafanyiwe mpango wa kupewa hati za umiliki,"alibainisha
Kunenge.
Licha ya maagizo
hayo ,pia atafanya kikao na baadhi ya wawakilishi wa wananchi,
msimamizi wa mirathi,familia na Mkuu wa Wilaya ili kuona namna ambavyo
wananchi hao watalipa kwa utaratibu maalum na wenye kufaa.
Alisema
,baada ya utaratibu huo kukamilika wananchi hao watapata huduma muhimu
ikiwa ni pamoja na maji na umeme huku akiwasisitiza wananchi kufuata
sheria na taratibu pale wanapotaka kununua na hata kujenga nyumba zao.
Vilevile
Kunenge alieleza,jambo ambalo limeamriwa na Mahakama hakuna anayeweza
kutengua wala kuingilia isipokuwa hatua nyingine ya Kimahakama(Rufaa) na
kwamba kinachotakiwa ni utekelezaji wa Mahakama .
Aliongezea,
Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ipo katika
kuwasaidia wananchi na ndio maana amefika eneo hilo kutatua mgogoro huo
kwa kuzingatia taratibu na misingi ya kisheria.
Nae
msimamizi wa mirathi ,Salim Mgombeo,alielezea anachotaka waliogoma
kulipa waondoke lakini waliokubali kulipa wabaki na kwamba mgogoro huo
ni mkubwa.
Baadhi ya
Wananchi hao, akiwemo Amina Azizi na Hassan Ng'anzi,wanasema wapo tayari
kulipa na wameomba Serikali iweke utaratibu maalum ambao utawawezesha
kulipa bila usumbufu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...