Na Abdullatif Yunus - MichuziTV Kagera.

Kampuni ya Utoaji Huduma katika Matukio ya Kijamii, Ijulikanayo kama JOLYN EVENTS  Imetambulishwa Rasmi Mkoani Kagera Aprili 23 Mwaka huu katika Hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Posta zilipo Ofisi za Kampuni hiyo.

Tukio hilo lililohudhuriwa na Wageni waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa Matukio,  limehusisha utambulisho wa huduma za kampuni hiyo ambayo licha ya kuonekana kutoa huduma mbalimbali lakini pia,  Jolyn Events wamejipanga kutoa huduma kwa ubora zaidi na kwa Viwango vya hali ya Juu.

Akitaja baadhi ya Huduma zitakazokuwa zikitolewa Meneja wa Kampuni ya Jolyn Mkoani Kagera Ndg. Best Julius amesema huduma hizo ni pamoja na Huduma ya Mapambo inayojumuisha Viti vyenye ubora, mahema ya kisasa, mazuria, keki washeeheshaji n.k pia huduma ya Uratibu na Uandaaji wa Matukio ya aina zote mfano Harusi, matamasha n.k

Meneja Julius Ameongeza kuwa Kampuni ya Jolyn itaendelea kuboresha huduma za Mazishi na ndio maana Kampuni inalo Gari la Kubeba na Kusafirisha Mwili wa Marehemu, Mashine ya Kushusha Mwili wa Marehemu Kaburini, mashada pamoja na Kuscan picha ya Kigae  au Kioo ya Marehemu.
Hata hivyo Kampuni hii imesogeza huduma ya Vyoo vya Kuhamisha maarufu kama Mobile Toilets sambamba na Usafiri wa kukodi wa kubeba Abiria na Mizigo.

Mgeni Rasmi katika hafla Hiyo Diwani wa Kata Bilele Mhe. Tawfiq Sharifu aliyemuwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa, amepongeza namna ambavyo Kijana Mwekezaji Joas Rwegoshora licha ya kuishi Ulaya muda mrefu kaamua kurudi Kuwekeza Bukoba na hivyo kuwataka Vijana wengine kuiga mfano huo.

Tayari kampuni Imeanza kutoka Huduma huku Meneja akitangaza Ofa ya Nusu bei kwa Wateja wa Mwanzo.










 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...