Raisa Said,Tanga
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka wakuu wa wilaya na maofisa
lishe mkoani humo kufanya tathmini na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu
suala la lishe.
Aidha amewataka maofisa lishe kutoa elimu kwa
wajawazito kuhusu lishe bora na vyakula mbadala sahihi vya dawa za
kuongeza damu ili aendelee kuwa salama katika kipindi cha ujauzito pindi
anapokosa dawa za kuongeza damu katika kituo cha afya au hospitalini.
Malima amesema hayo jana jijini Tanga, katika kikao kazi cha kutathimini utekelezaji mkataba wa lishe kipindi cha nusu mwaka.
"Kuna
maelekezo ambayo serikali imetoa, si maelekezo ya masikhara kuna siku
mtakuja kuulizwa na ninyi wakuu wa wilaya ndiyo wenye kusimamia suala la
lishe, mkakae na watu wenu wawape tafsiri na uelewa kuhusu lishe kisha
tutakuja kujadili kwenye kikao kijacho kama hiki. Tusifike sehemu ambayo
tutakuja kuulizwa suala la lishe.
"Mkishakuwa na uelewa wa
pamoja ninyi maofisa wa lishe tunaomba mtuainishie uhusiano kati ya
lishe na akili za darasani. Maana kama tunataka Tanga iwe na watoto
wenye akili basi tuwe na lishe bora na kama mnashindwa kufikia malengo
kwa sababu hamna fedha za kutosha mseme." alisema Malima.
Pamoja
na mambo mengine, Malima alisema wanaotoa elimu ya lishe kuwaambia watu
vyakula au matunda wanayokula yanawasaidia nini badala ya kuwasisitiza
kula aina fulani za vyakula huku akiwataka wananchi mkoani hapa kutumia
simu zao kuangalia na kujifunza masuala ya lishe.
Awali akitoa
tathmini ya lishe ya Mkoa wa Tanga, Ofisa na Mratibu wa Lishe wa mkoa,
Mwanamvua Zubeir alisema mkoa unakabiliwa na tatizo la udumavu ambapo
asilimia 34 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa ambapo alishauri
halmashauri zote kuwekeza katika lishe kwa sababu lishe ndiyo msingi wa
afya njema ya jamii lakini pia nguvukazi ya taifa lenye kuwa na maamuzi
yenye kuzalisha.
"Tatizo la udumavu haliathiri tu kimo kwamba mtu
ataonekana mfupi lakini maana yake hata ukuaji wa ubongo wake umedumaa.
Udumavu unaathiri hata mtoto kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo
yake darasani akiwa mwanafunzi lakini hata akiwa mkubwa ubongo wake
unakuwa hauna maamuzi mazuri ya busara katika jamii.
"Ukuaji wa
ubongo unaanzia mtoto akiwa tumboni kwa maana kwamba ili tuwekeze
kurekebisha suala la udumavu ni lazima tuwekeze katika lishe ya mama
kuanzia anapokuwa .jamzito hadi mtoto atakapozaliwa na kufikisha miaka
miwili, hizo tunahesabu ni siku 1,000 yaani kuanzia mimba inapotungwa
hadi umri wa miaka miwili baada ya hapo tukimpa mtoto virutubishi
tunaweza kurekebisha mambo mengine lakini si ulemavu. Kwa hiyo hiki
ndiyo kipindi muhimu zaidi kuwekeza katika suala zima la afya ya mtoto,"
amesema
Hata hivyo Serikali kupitia Program Jumuishi ya Malezi
,Makuzi na Maendeleo ya awli ya mtoto (PJT-MMMAM 2021/22-2025/26 )
Imeelezwa Jitihada za kushughulikia Hali ya lishe ya watoto nchini
zimekuwa na mafanikio malubwa kupitia afua maalum za kuboresha lishe
(Scaling Up Nutrition- Sun) ambazo ni harakati za kimkakati
zinajumuisha wadau mbalimbali.
Japokuwa karibu watoto wote
asilimia 96.6 wenye umri wa miezi 0-23 wamewahi kunyonyeshwa ,Bado ipo
haja ya kuboresha Kwa kuanza kunyonyesha mtoto saa moja baada ya
kuzaliwa ni asilimia 53.5. vilevile unyonyeshaji pekee wa maziwa ya mama
Kwa watoto wa miezi 0-6 ni asilimia 58.
Pia Kuna upungufu mkubwa
wa unyonyeshaji katikamwaka wa pili ,ambapo asilimia 92.2 ya watoto
waliendelea kunyonyeshwa Kwa mwkaa wa kwanza ikishuka hadi asilimia
43.3 Kwa miaka miwili kama inavyopendekezwa. Wakati huo huo asilimia 92
ya watoto wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi 8 walianzishiwa vyakula
vya ziada Kwa wakati inafaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...