NA FARIDA SAID MICHUZI TV.

Asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za binadamu nchini, zimeitaka serikali kutilia mkazo utekelezaji wa mapendekozo 187 yaliyoridhiwa katika Tathimini ya hali ya haki za binadamu kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, hasa katika uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Hayo yamelezwa mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Bodi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Bi. Sophia Komba wakati akifungua kikao kazi cha kujadili maandalizi ya mpango ufuatiliaji wa mapendekezo yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha maandalizi ya mpango wa kufuatilia Mapendekezo yaliyokubaliwa na Tanzania katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, Bi. Sophia amesema kati ya mapendekezo 252 yaliyo wasilishwa na nchi mbalimbali, Tanzania iliridhia jumla ya Mapendekezo 187, kikao hicho kinalenga kufanyia tathimini ya namna ya utekelezaji wake.

Pia Bi.Komba amesema moja ya mapendekezo ambayo Serikali yameikubali ni pamoja na watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo yao lengo likuwa ni kumpa mtoto wa kike haki ya kupata elimu.

“Tunashukuru kukubaliwa kwa pendekezo hili maana tunaona nguvu kazi kubwa ya mtoto wa kike huwa inaachwa nyuma bila ya kuendelea na shule kwa sababu ya ujauzito na kuna sababu nyingi sana zinzaomfanya mtoto wa kike apate ujauzito hivyo tunaona ni kumnyima mtoto huyu haki yake ya kupata elimu.”Alisema Bi Komba.

Amesema pendekezo lingine lilikuwa ni kuangalia upya sheria ya vyombo vya habari ambayo imekuwa ikiminya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza hali inayosababisha wananchi kukosa taarifa kwa wakati.

Ameongeza kuwa kufanyiwa kazi kwa mapendekezo hayo kutatoa fursa kwa wananchi kupata haki zao za msingi ikiwemo haki ya kupata habari huku washiriki wa kikao hicho kutoka asasi mbalimbali za kiraia ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Save the Children wamesema kuna umuhimu wa kuwepo kwa mpango shirikishi katika utekelezaji wa mapendokezo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya huduma za kisheria kutoka Tume ya haki za binadamu na utawala Bora Bwana Nabor Assey , amesema pamoja na kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyo kwisha ridhiwa, pia wanapitia upya mapendekezo yaliyo baki.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimelenga kupitia mapendekezo yaliyokubaliwa na jamhuri ya muungano wa Tanzania Novemba 2021, katika kikao cha 49 cha baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, kuandaa mpango wa pamoja wa kufuatilia mapendekezo hayo yaliyo kubaliwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...