KITUO cha Uwekezaji Tanzania TIC leo kimetembelea mradi wa Kamaka Industrial Park wa kongani ya viwanda uliopo Mlandizi Kibaha
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema mradi huo unatarajia kuwekeza kiasi cha shilingi za Kitanzania zaidi ya bilioni 60 na unatarajia kuajiri zaidi ya watu 5000 moja kwa moja mara utakapokamilika.
Mradi huo unatarajia kujengwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza inahusisha miundombinu ya barabara, maji, umeme, uzio na majengo ambapo awamu hiyo ya kwanza imekamilika kwa asilimia zaidi ya 55% alisema Dkt. Kazi.
Amesema mradi utaongeza mapato ya serikali kwa kuongeza wigo wa kodi lakini pia ujenzi wa viwanda utarahisisha upatikanaji wa bidhaa mbalimbali.
Yusuph Manzi mmoja wa Wakurugenzi wa Kamaka amesema mradi huo unaonyesha dhamira ya dhati kwa Watanzania kuunga mkono serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa kongani za viwanda.
Alisema mradi utakamilika kwa muda uliopangwa na ni matarajio yao mradi utachagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mkoa wa Pwani.
Mradi huo upo kwenye eneo la ukubwa wa ekari 1000 na awamu ya kwanza ya ujenzi inatarajia kukamilika ifikapo Desemba 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...