Na.Khadija Seif, Michuzi TV
MRADI wa Usalama Barabarani unatarajia kuwanufaisha Shule za Msingi 11 za jiji la Ilala mkoani Dar es salaam na kuboresha Miundombinu ya vivuko.
Akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kuzindua, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi Mukadam Mukadam Amesema ametoa pongezi Kwa Taasisi hiyo kwa kusaidia watoto Kwa takribani shule 11 na kuendelea kuwa salama kwani linashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha na usalama Barabarani unazingatiwa.
"Hali ya usalama Barabarani ni shwari japo Kuna changamoto za ajali ambazo Madereva wengi hawafati Sheria na kufanya uzembe wa kutofata alama sahihi na undeshaji usio salama hivyo jeshi la polisi litahakikisha na linaendelea kuwa imara lengo kupunguza ajali za Barabarani hususani Kwa watoto Mashuleni."
Aidha, Mukadam ameeleza pia Jeshi la polisi likishirikiana na wadau wa usalama Barabarani linaendelea kutoa Elimu Kwa kundi la Madereva wa bodaboda kuona Kwa jinsi gani wanafata sheria na alama zote za kiusalama Barabarani katika Mikoa yote nchini.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari (AAT) Nizar jivani amesema Ajali za Barabarani zimekua zikiongezeka na kusababisha vifo na majeruhi Kwa nchi nyingi ikiwemo Tanzania .
Jivani ameeleza Kwa namna Mradi huo ambao uliwapa fursa ya kuweka alama za Barabarani hasa kwenye Maeneo ya shule.
"Tumeweza kuweka nguzo za alama za usalama la vile 30km,alama ya punguza mwendo,alama ya pundamilia na alama ya simama.
Ameongeza kuwa ametoa wito Kwa jeshi la polisi kutengeneza alama Kwa Madereva wa bodaboda Ili ni alama ya kuonyesha mahali wanapotokea Ili kuweza kugundua ni sehemu gani au Madereva wa kitongaji kipi ni wavunjifu wa sheria Barabarani.
Picha ya pamoja wakiwemo Viongozi mbalimbali akiwemo Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi Mukadam Mukadam ,Rais wa Mashindano ya Mbio za Magari (AAT) Wanafunzi na walimu kutoka shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Shaban Robert wakishiriki kikamilifu utambulisho wa Mradi wa Usalama Barabarani wilaya ya ilala jijini Dar es salaam ulioandaliwa na Taasisi ya michezo ya Mbio za Magari.
Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi Mukadam Mukadam akizungumza na Waandishi Wahabari mara baada ya kutambulisha rasmi Shule 11 nufaika zilizopatiwa Mradi wa Usalama Barabarani wilaya ya ilala jijini Dar es salaam
Mmoja wa wadhamini wa Mradi wa Usalama Barabarani Kampuni ya maziwa ya Asas akipokea Cheti Cha ushiriki kutoka Kwa Rais wa Mashindano ya Mbio za Magari Nizar jivani (AAT) mara baada ya kutambulisha rasmi Mradi nufaika wa Usalama Barabarani Kwa shule 11 jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...