Meridianbet kwa kutambua madhara makubwa ya ugonjwa wa Malaria kwa wanajamii,
imetumia fursa ya siku maalumu ya maadhimisho
ya Malaria Duniani (Aprili 25, 2022) kuifikia jamii na hasa watoa huduma ya
afya ambao ni watu muhimu katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Kwa kutambua umuhimu wa watoa huduma wa Afya, Meridianbet iliitembelea Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Amana
ilikujumuika pamoja na watendaji wa hospitali hiyo katika jitihada adhimu za
kuilinda na kuiokoa jamii kwenye janga la ugonjwa wa Malaria.
Hii imeendelea kuwa desturi na utamaduni wa Meridianbet kuifikia jamii kwa namna tofauti tofauti lengo likiwa
ni kurudisha kwa jamii inayoizunguka. Ni dhahiri kuwa, Meridianbet pekee
haiwezi kutatua changamoto au kuzifikia jamii zote zenye uhitaji na,
kwakutambua hilo, Meridianbet wamekuwa wakishiriki na kuchangia kwenye matukio mbalimbali
kadiri ya uwezo wao kwa wakati husika. Imani kubwa ya kampuni hii katika
utaratibu huu ni kuisaidia jamii kwa kidogo kinachowezekana ili kwa pamoja,
jamii zote ziwezekutekeleza majukumu yao ya kila siku zikiwa katika mazingira
salama na wezeshi kiutelekezaji.
Mazingira ni kielelezo kimojawapo kinachohusiana moja kwa moja na
kuenea kwa ugonjwa wa Malaria. Hili hudhihirika katika maeneo ambayo mazingira
sio masafi na salama kwa jamii inayoishi au kutumia eneo hilo. Kwa kutambua
umuhimu wa Mazingira, Meridianbet imechangia
baadhi ya vifaa vya usafi wa mazingira kwa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Amana
ili kuiongezea nguvu hospitali hiyo kwenye muendelezo wa ufanyaji usafi kwenye
mazingira yanayoizunguka. Pamoja na vifaa vya usafi, pia imechangia baadhi ya
vifaa tiba ambavyo vitaongeza nguvu kwenye utoaji wa matibabu kwa jamii
inayofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu mbalimbali.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa wawikilishi wa Kampuni
ya Meridianbet, Afisa
Mahusiano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, Ndugu. Suphian Mndolwa, ameishukuru kampuni ya Meridianbet kwa kuitembelea hospitali
hiyo na kuiongezea nguvu kwenye vifaa vya kiutendaji kazi hospitalini hapo.
Aidha, ameongezea kuwa, bado hospitali hiyo inaendelea kuiasa jamii kujitokeza
kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa
maisha ya watu wengi nchini wenye uhitaji wa damu ikiwa ni pamoja na kuiomba kampuni ya Meridianbet kuendelea kuwa
karibu na jamii kwani, kwa kidogo wanachokirudisha kwa jamii, kinaokoa maisha
ya wanajamii wengi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...