



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackaon (Mb), amewataka Wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao na si kuiachia Serikali kuu pekee.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Aprili 16, 2022 katika hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ‘UWT’ Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya kwa lengo la kumpongeza Mhe. Rais Samia pamoja na Mhe. Spika Dkt. Tulia kwa kuchaguliwa kushika nafasi za juu za Uongozi nchini.
“Ndugu zangu, sote tunatambua ya kwamba nchi yetu imekuwa ikipiga hatua za kimaendeleo kila kukicha katika kuhakikisha inaboresha miundombinu yetu kama vile sekta za afya, elimu pamoja na elimu. Kwa hakika Serikali pekee haiwezi kuyakamilisha yote kwa wakati hivyo ni jukumu letu sisi Wananchi pia kuiunga mkono” amesema DKt. Tulia
Mhe. Spika amesisitiza kuwa, endapo kila mwananchi kwa nafasi yake ataamua kwa dhati kusimamia na kulinda miradi iliyoanzishwa na Serikali basi ni hakika taifa litakua kwa kasi huku akiwataka kila mmoja kuendelea kumuombea maisha marefu Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza taifa kwa amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...