NA FARIDA SAID, MOROGORO.
Shirika
la umeme nchini (TANESCO) limesema limejipanga kumaliza changamoto ya
hitilafu inayojitokeza mara kwa mara katika kituo cha kupokea, kupoza
na kusambaza umeme cha Msamvu (Msamvu Substation) mkoani Morogoro kwa
kununua vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kubaini hitilafu kabla
haijatokea na kuathiri miundombinu ya Shirika hilo.
Akizungumza
Mjini Morogoro mara baada ya kutembelea na kujionea kazi zinazofanywa
na mafundi wa TANESCO katika kituo cha Msamvu za kuhakikisha hali ya
upatikanaji wa umeme inaimalika mkoani Morogoro na maeneo ya jirani
kutokana na kuungua kwa kituo hicho Mkurugenzi wa TANESCO Bwana. Mharage
Chande amesema shirika litaongeza vitendea kazi na tayari shirika hilo
limeanza kufanya tathimini ghalama ya kufanya matengenezo ya mashine
umba (Transfoma ) kubwa zote nchini ili kuona ni kiasi gani kitatumika
katika kufanya matengenezo.
Amesema
kutokana na Mkoa wa Morogoro kuwa tegemezi katika uzarishaji wa mazao
ya chakula na biasharana pamoja na uwepo wa viwanda kumeufanya Mkoa
kuwa na matumizi makubwa ya nishati ya umeme hivyo TANESCO ipo katika
mpango wa kuongeza kituo kingine cha kupokea, kupoza na kusambaza
umeme ambacho kitakuwa kikubwa zaidi.
Aidha
amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuacha kupeana lawama kufuatia
matukio ya kuungua kwa kituo cha Msamvu badala yake wafanye kazi na
kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora ya nishati ya umeme.
Kwaupande
wake msemaji wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Martin Mwambene
amesema kazi ya kusafirisha mashine umba (Transfoma) kutoka kwenye
kituo cha Zuzu mkoani Dodoma mpaka Msamvu limekamilika na kinachendelea
ni zoezi la kuifunga Transfoma hiyo ambapo amsema kazi ya kufunga
Transfoma itakamilika hivi karibuni.
PIA
amesema kuungua kwa kituo cha Msamvu kumesababisha mikoa ya Kaskazini
kukosa umeme wa uhakika kutokana na kuzidiwa kwa njia za kusafirishia
umeme katika kituo cha Chalinze ambacho awali kilikuwa kinatumika
kusafirisha umeme wa mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro huku akiwatoa
hofu wakazi wa maeneo hayo kuwa nishati hiyo itarudi katika hali ya
kawaida baada ya kukamilika kwa matengenezo katika kituo cha Msamvu.
Ikumbukwe
kuwa Agost 2, 2021, Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Msamvu mkoani
Morogoro kilipata hitilafu iliyosababisha kuwaka moto kwa jumba la
kudhibiti mifumo ya umeme wa msongo wa kilovolti 33.
Aliyekuwa
Wziri wa Nishati Dk Kalemani aliagiza kuwasimamisha kazi watumishi
watatu wa Shirika hilo mkoani Morogoro wakipisha uchunguzi
utakapomalizika ambao uchunguzi huo pia unamhusisha na mfanyakazi
mwingine mmoja wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Mwendokasi
(SGR).
Licha ya kuchukua
hatua hizo pia alitembelea eneo Tungi, Manispaa ya Morogoro ilipo
kebo ya umeme ambapo inapodaiwa ni chanzo cha kuungua moto jengo la
mitambo katika kituo hicho.
Ni kutokana na
kukatwa kwa bomba lenye kebo iliyochimbiwa chini ya ardhi ambayo
inaunganika na kituo hicho kufuatia mtambo wa kuchonga barabara
(Burudoza) ya kampuni ya Yapi Merkezi iliyojenga reli ya mwendo
kasi(SGR) kukatwa kwa kebo hiyo .
Kwa
mujibu wa Waziri wa Nishati , moto huo umesababisha hasara ya
zaidi ya Sh bilioni mbili na kukosekana kwa huduma ya umeme wa uhakika
mkoani humo.
Kufuatia
tukio hilo , Augosti 14, 2021 , Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania
Kassim Majaliwa, alipotembeela kituo hicho aliuangiza Uongozi wa Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya mapitio ya wataalamu wote
wanaosimamia vituo 51 vya kupokea na kupoza umeme nchini.
Alisema lengo ni kuona kama wanakidhi vigezo na kuona kama wanafanya kazi kwa weledi kutokana na kusimamia mitambo hatari .
Pia
tukio la pili lilitokea Aprili 13, 2022 kwa mashine umba (Transfoma )
iliyoko kwenye Kituo cha Kupokea na kupooza umeme cha Msamvu kuungua
moto na kusababisha sehemu kubwa ya amkoa wa Morogoro na mikoa jirani
kukosa huduma ya umeme .
Licha
ya maeneo ya wilaya za mkoa huo pia kuungua kwa mashine umba hiyo
kulisababisha mikoa Jirani ikiwemo Pwani , mikoa ya kanda ya Kaskazini
na Dar es Salaam iliathiriwa.
Kwa mujibu wa uongozi wa Taneseco kwa sasa kunavituo 51 vya kupokea na kupoza umeme Nchi nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...