
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela amelitaka shirika la ugavi wa Umeme Tanzania Mkoa wa Morogoro kuhakikisha linaongeza kasi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara ili kukipunguzia mzigo Kituo cha kupoza umeme cha Msamvu kutokana na kituo hicho kupata hitilafu ya umeme mara tatu sasa tangu tukio la kituo hicho kuwaka moto Mwezi Agosti 2021.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai hiyo baada ya moja ya transforms kubwa katika kituo cha Msamvu Manispaa ya Morogoro leo majira ya mchana kupata hitilafu na kuwaka moto.
Shigela amesema Transforma iliyopata hitilafu na kuwaka moto ni moja na ililetwa baada ya tukio la moto la 2021 huku chumba cha kuendesha mitambo kituoni hapo ambacho hakikuungua katika tukio ndicho kimewaka moto, ndipo akatoa rai kwa TANESCO kufanya jitihada za makusudi kudhibiti kutokea kwa ajali ya moto mara kwa mara katika kituo hicho.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mhandisi Fedgrace Shuma amesema kwasasa bado wataalamu wanafanya tathimini kubaini kiwango cha madhara yaliyojitokeza pamoja na kufanya jitihada za kurejesha huduma ya umeme yaliyoathirika
Maeneo yaliyo athirika kutokana na hitilafu hiyo ni maeneo yote ya mji wa Morogoro na huduma ya umeme itarejea kupitia kituo cha umeme cha Chalinze.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...