Na Farida Mangube, Morogoro.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini (TAWA) imewataka askari wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa kufuata sheria na nidhamu ya kijeshi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuepuka kuwanyanyasa wananchi, kuondoa migogoro baina yao na wananchi, kuepuka vitendo vya rushwa pamoja na kuzuia kuvamiwa maeneo ambayo yapo chini ya mamlaka hiyo.

Hayo yamebainishwa Mkoani hapa na Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA) Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko mara baada ya kuwatunuku na kuwavisha vyeo makamishina wasaidizi wandamizi watano na makamishina wasaidizi kumi na mbili wa askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini (TAWA).

Aidha Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko amesema kupitia askari ambao wametunukiwa na kuvishwa vyeo, TAWA inategemea kuona mabadiliko makubwa katika maeneo yote ambayo yanasimamiwa na askari hao hasa katika kuishi vizuri na wananchi ili kuondoa migogoro inayojitokeza baina yao na wananchi.

Hata hivyo Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko amesema kuwa bodi ya TAWA na Menejimenti yake inategemea kuona askari wa TAWA wakitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na nidhamu kubwa ya kijeshi.

“Huko mnakokwenda tunategemea kuona mabadiliko makubwa, hatutegemei kuona migogoro ya wananchi, hatutegemei kuona kwamba maeneo yetu yanavamiwa, hatutegemei kuona wananchi wananyanyaswa bila ya sababu, hatutegemei kuona maeneo yetu yanavamiwa, hatugemei kuona rushwa, sisi bodi na menejimenti muhakikishe ya kwamba mnakaa vizuri na wananchi, mhakikishe vijana wenu wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na nidhamu ya kijeshi” Amesema Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA).

Kwa upande wake Kamishina Uhifadhi Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amewataka makamishina wasaidizi wandamizi watano na makamishina wasaidizi kumi na mbili wa askari wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA) ambao wametunukiwa na kuwavishwa vyeo kuchapa kazi kwa ujasiri na weledi wa hali ya juu ili lengo la serikali la kuanzishwa kwa jeshi la uhifadhi litimie.

Kamishina Uhifadhi Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amewataka makamishina hao kuhakikisha wanaongoza kwa ufanishi katika usimamizi wa ulinzi wa rasilimali.

Vilevile amesema kuwa TAWA inatekeleza miradi thelathini na mbili kupitia fedha za maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Maendeleo dhidi ya uviko 19, hivyo amewataka makamishina hao kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama serikali ilivyoelekeza kuwa mwezi juni mwaka huu miradi yote hiyo iwe imekamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

“Tumieni weledi, uaminifu, umahiri na vipawa vyenu vyote kuhakikisha kwamba miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ubora unaokusudiwa”. Amesema Kamishina Uhifadhi Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi Major Jenerali Mstaafu George Msongole amewataka makamishina ambao wametunikiwa na kuvishwa vyeo kuhakikisha kila mmoja anajitambua ili kupata mafanikio mengi kutoka kwao ambayo yataleta mapinduzi chanya.

Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA) Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko, akimtunuku na kumvisha Cheo, hafla ambayo imefanyika mkoani hapa. Picha na Farida Mangube. 

Kamishina  Uhifadhi Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, akiongea mara baada ya hafla ya  kuwatunuku na kuwavisha vyeo baadhi ya askari wa Tawa kuwa  makamishina wasaidizi wandamizi  na makamishina wasaidizi, hafla ambayo imefanyika mkoani hapa. Picha na Farida Mangube.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi Major Jenerali Mstaafu George Msongole  akiongea mara baada ya hafla ya  kuwatunuku na kuwavisha vyeo baadhi ya askari wa Tawa kuwa  makamishina wasaidizi wandamizi  na makamishina wasaidizi, hafla ambayo imefanyika mkoani hapa. Picha na Farida Mangube.

Baadhi ya makamishina wasaidizi wandamizi  na makamishina wasaidizi wa askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini (TAWA), wakiwa tayari wametunikiwa na kuvishwa vyeo na Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA) Major Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko mkoani Hapa. Picha na Farida Mangube.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...