Na Pamela Mollel,Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO),Mhandisi Frederick Kahimba amesema wamebuni Teknolojia mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali zitakazo wezesha watanzania kuagiza vifaa hivyo hapa nchini

Aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza na kuandika habari za Sayansi na Teknolojia iliyofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania(COSTECH)

Alisema kuwa Teknolojia hizo ni pamoja na Majokofu ya kuhifadhi miili,Vitanda vya kujifungulia kinamama na viteketeza taka katika hospitali

"Taasisi hii imekuwa ikibuni vifaa mbalimbali vya hospitali na asilimia 80 ya vifaa hivi vinaagizwa nje ya nchi,ni fursa kwa watanzania kuchangamkia hili kwa kuagiza hapa nchini "alisema Kahimba

Injinia Kahimba alisema kuwa uwepo wa vifaa hivyo hapa nchini itasaidia watanzania kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo

Aliongeza kuwa wanashukuru COSTECH kwa kuwawezesha fedha za kufanya utafiti kiasi cha shilingi milioni 128na kati ya hizo milioni 65 walitumia kwaajili ya mtambo wa kusafishia mafuta ya alizeti.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania TEMDO,Injinia Fredrick Kahimba akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uwepo wa vifaa mbalimbali vya hospitali vinavyotengenezwa na Taasisi hiyo

Fundi mahiri wa kutengeneza vitanda vya chuma kwaajili ya matumizi ya hospitali Flora Kweka akiwa katika majukumu yake.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...