Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katika kuhamasisha uwekezaji nchi na kuchochea uwekezaji na ukuaji wa uchumi Kituo cha Uwekezaji cha Nchini(TIC) kimesajili miradi 85 kutokea mwezi januari mpaka machi mwaka huu ambayo itasadia katika kuzalisha ajira na kukuza pato la Tiafa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt.Maduhu Kazi amesema kiwango hicho ni kikubwa kulinganisha na idadi ya miradi 51 kwa kipindi cha mwaka 2021 ambapo ajira 12,191 zinatarajiwa kuzalishwa.
“Miradi hiyo inathamani ya Dola za Marekani milioni 787.40 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka 2021 ambapo thamani ya miradi ilikuwa dola milioni 450.56 sawa na ongezeko la asilimia 74.76
Alisema miradi hiyo imelenga katika uwekezaji kwenye sekta ya usafirishaji, Viwanda, miundombinu, kilimo ujenzi/majengo ya biashara, taasisi za fedha, rasilimali watu,utalii na huduma mbalimbali.
Alitaja baadhi ya kampuni zilizowekeza nchini ni pamoja na Taqa Arabia Tanzania ltd itakayojenga vituo 12 vya ubadilishaji wa magari kutoka kutumia petrol na diseli kwenda kwenye mfumo wa gesi na utekelezaji wa vituo viwili vikubwa utakamilika mwaka huu.
“Mradi wa ujenzi wa viwanda vya cement utatekelezwa na kampuni ya Alotaib nad blak Bib na Prime cement wenye thamani ya doa milioni 113 ambapo ajira 1097 zinatarajiwa kuzalishwa kupitia mradi huo,”alisema Dkt.Maduhu
Sambamba miradi hiyo upo wa kuunganisha magari aina ya Howo utakaotekelezwa na kampuni ya Saturn Corporation ambapo kampuni hiyo ni ushirikiano katika ya Tanzania na Canada.
“Katika kuhakikisha upungufu wa mafuta unapungua au kuisha nchini tumeweza kusajili kampuni ya Organo Africa ambayo itakwenda kufanya uzalishaji wa mafuta ya kula tani 182,000 kwa mwaka na kugharimu dola za Marekani milioni 42.68,” alisema Dkt.Maduhu
Alieleza kuwa kiwanda hicho kitazalisha ajira za moja kwa moja 1,097 na kutengeneza soko kwa mazao mbalimbali ya wakulima nchni yatakayotumika kama malighafi ya kutengeneza bidhaa hiyo.
“Hizi ni juhudi za kituo katika kuhakikisha tunaibuwa fursa mbalimbali zilizopo na kuzitangaza kwa wawekezaji ndani na nje ya nchini ili wafanya uwekezaji ambao utakwenda kutatua changamoto mbalimbali ndani ya nchi hususani ajira kwa vijana,” alisema Dkt.Maduhu
Aidha Dkt.Maduhu alisema katika kipindi hicho pia wametiliana saini miradi 6 inayotarajiwa kuwekeza kiasi cha dola za marekani bilioni 1.1 ambapo itakwenda kutumika kukuza miradi iliyopo na kuanzisha miradi mipya ukiwemo wa ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha Intracom kinachojengwa Jijini Dodoma.
Aliwaeleza waandishi kuwa TIC itaendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali katika kuibuwa fursa na kuzitangaza kwa lengo la kuchochea uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi akizungumza kwenye mkutano na
waandishi wa habari, ofisini kwake Jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa
ya mafanikio ya uwekezaji kwa robo tatu ya mwaka (januari - machi 2022) ambapo jumla ya miradi 85
imesajiliwa na kituo hicho kulinganisha na miradi 51 iliyosajiliwa katika kipindi hicho kwa mwaka
2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...