Na Karama Kenyunko
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuna wakati ilikuwa inapitia katika wakati mgumu kutokana na wananchi kutoamini matangazo yake ya Utabiri wa Hali ya Hewa wanaoutoa kila siku ikiwa pamoja na matangazo misimu ya mvua inayotokea kila mwaka.

Imekuwa kawaida kwa wananchi kutoamini matangazo ya Utabiri wa hali ya Hewa yanayotolewa kutokana na kutoenda kama ilivyotabiriwa na TMA, hali iliyopunguza imani kwa mamlaka hiyo.

Hali hiyo imekuwa tofauti kwa siku za hivi karibuni kwani asilimia kubwa ya utabiri wa TMA umekuwa ukienda kama ilivyotangazwa hivyo taratibu imeanza kurudisha imani ya wananchi kwa mamlaka hiyo, iliyokuwa chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Wakati Tanzania kukiwa katika kipindi cha mvua za mwaka zinazoendelea kunyesha sehemu kubwa ya nchi, TMA imekuwa ikiendelea kutoa matangazo mbalimbali na hali inayoendelea ambayo kwa asilimia kubwa yametokea kama ilivyotabiriwa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (MB) amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dk. Agnes Kijazi kupitia kwa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka la Hali ya Hewa Tanzania kwa kuongeza usahihi wa taarifa zao za utabiri.

Prof. Mbarawa alitoa pongezi hizo alipokuwa anafungua Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ambao wanatoka katika mamlaka hizo nchi nzima Tanzania na Zanzibar.

“Nimfurahi kusikia kuwa mmeongeza viwango vya usahihi wa utabiri unaotolewa na kuongezeka kwa uelewa wa jamii kuhusiana na taarifa za Hali ya Hewa pamoja na mengine mengi; nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya,” alisema Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amesema anajua changamoto mbalimbali zikiwemo zile za maslahi duni, vifaa vya hali ya hewa na usafiri lakini wameweza kutekeleza udhibiti na uratibu wa shughuli za hali ya hewa kwa kiwango cha juu, wanastahili pongezi.

Amesema kutokana na utendaji wao huo, Waziri wameahidi kuendelea kuiwezesha Mamlaka kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo ili kutatua changamoto hizo na hivyo kuwezesha utekelezaji wa majukumu yenu kwa ufanisi zaidi ya iliyokuwa sasa.

Uwezo unaonyesha na TMA pamoja na changamoto wanazopitia kuna kila sababu ya kuipongeza mamlaka hiyo ambayo ilianza kupoteza matumiani na kufanikiwa kurudisha imani kwa wananchi kupitia utabiri wao wa Hali ya Hewa nchini.

Pamoja na ahadi za Serikali kupitia kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, lakini Mamlaka ya TMA imeshauriwa kutafuta vyanzo ya mapato kama vile ya tozo kutoka kwa taasisi zinazoshirikiana na mamlaka hiyo ili iweze kujiendesha katika shughuli zake mbalimbali.

Serikali itaiwezesha Mamlaka kuimarisha mfumo wa uangazi, bado kutakuwa na uhitaji wa fedha za uendeshaji wa mifumo hiyo, hivyo wanatakiwa kutumia vyema kanuni inayohusiana na mapato ili wakusanye mapato ya kutosha kwa ajili ya uendeshaji wa taasisi.

TMA ipo katika hatua mbalimbali za majadiliano ya kukubaliana tozo mpya kwa sekta nyingine, kama sekta ya Ujenzi, wamiliki wa vyombo vya majini na watalii, ambao wanatakiwa kuchangia.

Mamlaka ya TMA wametakiwa majadiliano yao yajikite kuwaelimisha wadau kuitekeleza sheria ya kuchangia huduma hiyo ni suala la kisheria hivyo kila mdau hana budi kulitekeleza.

Hali ilivyo sasa, kama TMA watapata msaada kutoka serikali ikiwa pamoja na kujiimarisha kutokana na tozo wanazostahili kuchangiwa, wataweza kujiendesha vizuri, hivyo kuweza kutoa huduma yao kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Utabiri wa hali ya hewa una masaada mkubwa katika jamii, mfano wakulima wanategemea taarifa sahihi za msimu mvua ii waweze kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu wa kilimo.

Mbali na wakuliwa, wasafiri kwa vyombo vya majini wanategemea hali ya hewa ili kujua hali ilivyo baraharini, ziwani na maeneo mengine ambayo itawasaidia kuweza kusafirisha vyombo hivyo na abiria kwa ujumla.

TMA ikiwezesha na kuimarika itaweza kufanya kazi kubwa zaidi yah ii ambayo itakuwa na mwanga mkubwa kwa wananchi katika shughuli zao mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...