Kutokana na changamoto ya ugonjwa wa kuweka mazingira rafiki ya kufundishia kwa njia ya masafa marefu kwa walimu wa vyuo vya ufundi stadi hapa nchini, kwa kununua vitendea kazi vitakavyo wasaidia walimu kufundisha wakiwa popote, hii itasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya walimu wa vyuo vya ufundi stadi hapa nchini walipokutana Mjini Morogoro kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo ya namna ya kufundisha kwa njia ya mtandao yalioandaliwa na shirika elimu sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa (UNESCO) kupitia mradi wake wa better education for Africa rise.
Wamesema kutokana na changamoto mbalimbali akiwemo ya uviko 19 kuna haja serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu wakiwemo UNESCO kuwekeza katika vitendea kazi vya kufundishia kwa njia ya mtandao kwani elimu ya masafa itawasaidia wanafunzi kuendelea na masomo hata pale zinapotokea changamoto zikiwemo za magonjwa ya kuambukiza.
“Tunaishukuru UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwani yatatusaidia kufundisha wanafunzi wengi Zaidi kwa wakati mmoja bila ya kukutana pia mihula ya masomo hayatavurugwa hata ikitokea majanga mbalimbali.” Walisema walimu hao.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo kaimu mkuu wa chuo cha walimu wa ufundi stadi Morogoro Bwana Andrew Boi amesema kuna uhuhimu wa kufundisha kwa njia ya mtandao katika vyuo vya mafunzo na ufundi stadi na kuiomba UNESCO kuendele kushirikiana na serikali ili vyuo vyote hapa nchini viwezi kutoa elimu kwa njia ya mtandao.
“kutokana na changamoto ya mlipuko wa magonjwa mbalimbali taasisi nyingi za TVET zitashindwa kutoa mafunzo kwa weredi kwa sababu mafunzo ya ana kwa ana yamekutana na chanamoto ya magonjwa ya mlipuko yanayosaa kwa njia ya hewa ana kugusana sasa.’ Alisema Bwana Boi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi kutoka Wizara ya elimu Daktari Noel Mbonde amesema elimu ya masafa itawapa fulsa walimu kufundishi wakiwa popote bila hata kuingilia darasani na kupunguza msongamano usikuwa wa lazima maeneo ya vyuo hasa katika kipindi hiki aambacho dunia inapambana na ugonjwa wa uviko 19.
“Hakuna ulazima wa mwalimu kwenda darasani na kuanza kufundisha unaweza kukaa ofisini kwako na ukafundisha na wanafunzi wakapata elimu kama kawaida.” alisema Dakta Mbonde
Aidha amewataka walimu hao waliopata mafunzo kuwa mabalozi wanzuri katika vyuo vyao ili kuendana na ukuaji wa teknoljia na kupambana na majanga mbalimbali yakiwemo ya magonjwa ya mlipuko ukiwemo UVIKO 19.
Mradi wa Better Education for Africa Rise ni Mradi wa miaka mitano unatekelezwa na shirika elimu Sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa (UNESCO) umeenza mwaka 2017 na kumalizika mwaka 2022 na kuwafikia walimu kutoka vyuo mbalimbali vya mafunzo na ufundi stadi hapa nchini .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...