Na Rhoda Ezekiel Kigoma
ZAIDI ya Wanafunzi 6000 wa shule za msingi mkoani kigoma, wamelazimika kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba katika umri mdogo kwa kipindi Cha mwaka wa masomo 2021.
Hayo yalibainishwa jana April 22 2022 na kaimu Afisa Elimu mkoa wa Kigoma , Devid Mwamalasi Wakati wa Uzinduzi wa shindano la uandishi wa Insha kwa wanafunzi wa shule za msingi ambalo limeandaliwa na shirika la World vision ambapo mikoa 13 ya Tanzania bara inatarajia kushiriki katika shindano Hilo.
Afisa huyo alisema katika kipindi hicho wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu za mimba kwa upande wa shule za msingi ni 6123 na sekondari ni 676 huku katika kipindi Cha miezi miwili ya January na February mwaka 2022 watoto 28 wa shule za masingi tayari wamelipotiwa kubeba mimba.
Aliongeza kuwa katika mkoa huo vipo vihatarishi mbalimbali vinavyopelekea baadhi ya watoto kubeba mimba ambapo amevitaja baadhi ya vihatarishi hivyo, kuwa ni pamoja na kukosekana kwa chakula shuleni hali inayopelekea watoto kujiingiza kwenye vishawishi, kutembea umbali mrefu na kuwepo kwa masoko ya usiku.
"Kwakweli mimba za utotoni ni changamoto katika jamii yetu lakini kikwazo kikubwa ni ukosefu wa chakula mashuleni watoto hawa hurazimina kujiingiza kwenye vishawishi mbalimbali hatimaye kuambulia kubeba ujauzito kwa sababu ya kutokuwa na chakula shuleni njaa ni kichocheo kikubwa Katika hilo" alisema Mwamalasi ambaye ni .
Akiongia kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la World Vision Nchin Vicent Kasuga ambaye pia ni meneja wa shirika hilo Kanda ya Iringa Ambao ndio wawezeshaji wa shindano hilo alisema malengo ya shindano hilo ni kuwajengea uwezo wa kujieleza wanafunzi wa shule za msingi na kukabilia na mimba za utotoni kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Aliongeza kuwa mimba za utotoni zinakatisha ndoto za watoto wengi wa shule za msingi na sekondari nchini, kwamba jamii inatakiwa kuungana na kukemea matendo hayo ili kujenga kizazi imara na chenye maono ili kuimalisha msingi wa maisha na maendeleo ya watu.
Alidai kuwa mbali na mimba za utotoni lakini pia kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto na kuwasihi viongozi wa dini pamoja na jamii kuendelea kukemea vitendo hivyo.
Akizindua shindano hilo mkuu wa wilaya ya Kigoma , Esther Mahawe kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Thobias Andengenye alitoa mwito kwa viongozi wa dini kukema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambavyo vimekuwa kichocheo kikubwa Cha mimba za utotoni.
Mahawe aliongeza kuwa serikali ya mkoa huo itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na mimba za utotoni sambamba na ukatili dhidi ya watoto mkoani humo na kupongeza shilika la World Vision kwa kuanzisha shindano Hilo ambalo litakuwa chachu ya vita dhidi ya mimba za utotoni.
"Sisi kama serikali ya mkoa wa kigoma tutaendelea kupambana kwa kutekeleza mikakati yote tuliyojiwekea ili kuhakikisha swala la mimba za utotoni zinakoma, kwakweli vitendo hivi, vinakatisha ndoto nyingi za watoto wetu" alisema mkuu wa wilaya ya Kigoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...